Jumanne, 18 Februari 2014

WAKRISTO 106 WAUWAWA KWA RISASI NA KUCHINJWA NIGERIA


Tokea 2014 ianze, zaidi ya Wakristo 130 wameripotiwa kuuwawa. ©CBN News
Unafanayeje, watu wanapozingira kijiji (mtaa) chenu na kuanza kuvamia kaya moja baada ya nyingine, kupiga risasi na kuchinja kooni wanaume wote wa kijiji chako? Unafanyeje pale ambapo kama wewe ni mwanamke na ukitaka kumtetea mwanaume yeyote, kuanzia mume, mtoto na hata mjukuu, basi nawe unauwawa? Na kisa cha haya yote ni kutakana na imani yako, kwamba tu umechagua kuwa Mkristo.
Tukio hili limetokea Kaskazini mwa Nigeria, ambapo watu 106, (wanaume 105 kati yao, na bibi mmoja aliyejaribu kumlinda mjukuu wake) wameuwawa kikatili kwenye kijiji cha Izghe, mwishoni mwa wiki hii.


Kwa mujibu wa shirika la habari la kikristo la BosNews Life, takriban waasi wapatao 100 wa kundi la Boko Haram, kama ambavyo wametambuliwa na vyombo vya usalama vya nchini humo, walikizingira kijiji cha Izghe usiku wa Jumamosi na kisha kuanza kushambulia kila mwanaume waliyemtia machoni, na kisha baada ya shambulizi hilo, kupita nyumba hadi nyumba ili kuhakiki kama kuna yeyote waliyemuacha hai, ili kummaliza.



Kwa mujibu wa mashuhuda ambao walikuwa wakihojiwa na shirika la habari la Uingereza, BBC. Wanasema kuwa, shambulizi hilo lilifanyika kwa kutumia bunduki, ambapo kuna wengine waliuwawa kwa kuchinjwa kooni.



Wakristo wanaishi kwa mateso nchini Nigeria. ©BosNewsLife
Hadi kunakucha, miili mingi ilikuwa imelala hovyo kwenye maeneo ya kijiji hicho, ambapo waliosalimika walikimbia kujinusuru, huku hatama ya miili hiyo ikiwa haijajulikana maazishi yake yatakuwaje.


Kwa mujibu wa gavana wa eneo la Borno, ambalo kulikuwa na shambulizi lililopelekea kuuwawa kwa watu 30 mapema wiki iliyopita kwenye mji wa Konduga, Kashim Shettima, ameeleza hali ya eneo hiyo kuwa ya hatari, ambapo ameomba jeshi liongeze nguvu maeneo hayo kwa ajili ya usalama wa wananchi, ingawa siku kadhaa zilizopita jeshi liliamua kuondoka eneo hilo kutokana na kuvamiwa kwa kuviziwa na kisha 9 kuuwawa.


Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Rais Goodluck Jonathan hivi karibuni alifanya mabadiliko kwenye jeshi lake, kutokana na kutatizwa na hali ya amani inavyotoweka kila kukicha.


Boko Haram ni kundi ambalo limekuwa likiwatangazia Wakristo wa kaskanzini mwa Nigeria kuwa waondoke ili eneo hilo lijitenge na kuwa na mamlaka ya kiislamu, na kuongozwa na sharia kali za dini hiyo. Taifa la Marekani limeshatangaza rasmi kuitambua Boko Harama kama kikundi cha ugaidi (kilicho nje ya taifa hilo), na hiyvo kuwa tayari kwa ujibu wa sheria za nchi hiyo, kuchukua hatua muda wowote watakapoona inafaa.


Leo wameuwawa Wakristo 106 hapahapa Africa, matukio kama haya yanatupeleka wapi? Kama ni maombi, basi muda ndio huu wa kusimama nayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni