Jumanne, 11 Februari 2014

KUJUA KAMA JINA LAKO LIMEANDIKWA KITABU CHA UZIMA NI SHILINGI ELFU 20,000 TU


Nabii mchungaji Thomas Wahome. © courtesy
Ikiwa takribani miezi miwili tangu kujulikana kwa huduma ya mtume Lesego wa Afrika ya kusini kuwaagiza waumini wake kula manyasi sambamba na kuwafanyia maombi akiwa amewakanyaga migongoni, mambo bado yanaendelea kwa watumishi wa Mungu waliopo Afrika kushangaza ulimwengu kupitia huduma zao.
Askofu Thomas Wahome wa huduma ya Helcopter of Christ church jijini Nairobi nchini Kenya amekuwa akiwatoza waumini wake kiasi cha shilingi 1000 za Kenya sawa na shilingi 18,000 za Kitanzania ili awaambie kama majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima mbinguni ama la kwakuwa askofu huyo ananjia ya kuweza kuona katika kitabu hicho. Mwanamama mmoja aitwaye Sheila Mbaya amesema alipatwa na mshtuko alipoambiwa na rafiki zake wanaosali kwa mtume huyo kuwa majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima hivyo ni vyema hata yeye akijua kama atakaribishwa mbinguni au la kwakufika kanisani hapo.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Nairobian waliotoa taarifa hizo waliamua kupiga simu ya kwa mtume huyo ili kujihakikishia kama kweli kuna huduma hiyo ambapo baada ya kupiga alipokea mwanadada aliyejitambulisha kama mchungaji Salome ambaye alikiri kuwepo kwa huduma hiyo na kwamba kama mpigaji alitaka kuangaliwa jina lake katika kitabu hicho alitakiwa kulipa shilingi 1,100 za Kenya sawa na shilingi elfu 20, 686 za Tanzania.

Ambapo mpigaji alitakiwa kutuma pesa hiyo kupitia namba 07XX032000 (namba za mwanzo zimefichwa) kisha afike kanisani hapo kesho yake majira ya saa 4 asubuhi ili askofu Wahome amweleze kama jina lake lipo katika kitabu cha uzima au la. Mtume huyo inaelezwa si mara ya kwanza kuwa na huduma za namna hiyo ambazo amekuwa akichukua pesa za waumini wake ambao inadaiwa wana hali duni kimaisha ambapo inadaiwa aliwahi kuwatoza waumini wake shilingi 1200 za Kenya ambazo ni zaidi ya elfo 20 za Kitanzania kwa kuwaambia yeyote atakaye gusa vazi lake atakalokuwa amevaa atapona matatizo yake kama ilivyokuwa kwa mwanamke aliyetokwa na damu kwa miaka 12 kama inavyoelezwa kwenye kitabu cha Marko mtakatifu 5:21-34
Kumekucha waumini, ni wakati wa kukaa macho sana na injili inayopatikana katika baadhi ya makanisa na huduma duniani. Hivi ni kweli kabisa nabii anauwezo wa kujua haya yote??? maana najua ni Mungu mwenyewe ajuaye na si mwanadamu awaye yeyote, nabii huyu ametoa wapi hili? Unasemaje juu ya huduma hii?

Hapa mwangalie katika moja ya huduma zake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni