Alhamisi, 27 Februari 2014
PICHA ZA AJALI MBAYA YA GARI ALIYOPATA MCHUNGAJI WA KANISA LA SABATO DODOMA
Mchungaji Michael Zacharia Twakaniki (katikati)akiwa hospitalini huko Dodoma kushoto mwenye tai ni Mhazini wa jimbo la Mashariki mwa Tanzania katika kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania Athanas Sigoma alipomtembelea juzi.Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Dodoma Michael Zachariah Twakaniki alipata ajali Februari 25,2014 ya gari ambalo alikuwa akiliendesha akiwa na abiria wenzake 6,wawili wakiwa ni watoto wake,wajukuu wawili na rafiki zao wawili.
Jumatano, 26 Februari 2014
SOMO : MAONO NA NDOTO *sehemu ya kwanza *
Jumamosi, 22 Februari 2014
WARAKA KWA FILEMONI * sehemu ya mwisho *
Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe...
Jina la Bwana libarikiwe...
Walaka kwa Filemoni ni kitabu kizuri sana ambacho ndani yake yapo mafunuo mengi ya kujifunza.
Ninajua ya kwamba kama utakuwa umebahatika kujifunza fundisho hili mahali hapa,
ni ukweli kabisa utakuwa umefaidi sana kwa kujua maana halisi ya walaka huu kwa Filemoni.
MUNGU KUWAHUDUMIA WATEULE WAKE KITUNDA .
Mama mchungaji Madembwe akiwa katika kumwabudu Mungu.
Maono ya mtumishi wa Mungu mama mchungaji Happyness Madembwe juu ya ibada ya sifa na kuabudu bado yanaendelea kutenda kazi ndani ya uwepo wa Mungu na kwa wale waliopata nafasi ya kuhudhuria ibada hiyo wamekuwa mashuhuda jinsi Mungu anavyo wahudumia watu wake.
SOMO: MATATIZO YA FAMILIA/UKOO
Na. Mch Josephat Gwajima
1 Mambo ya Nyakati 1:1-54
Ni kitabu cha kushangaza sana kwenye biblia sababu kinaelezea tu Fulani akamzaa Fulani, ni kitabu kilichokuwa inanipa taabu sana kukisoma kwenye biblia sababu majina mengine ni magumu hata kuyatamka, nikawa najiuliza hiki kitabu kinamaanisha nini na kwanini kimeandikwa kwenye biblia, nilikuwa sielewi ni nini mtu unaweza kujifunza kwa kuambiwa huyu akamzaa huyu.
Jumanne, 18 Februari 2014
SOMO : MIUJIZA YA WATU KUANGUKA CHINI NA ASKOFU KAKOBE
WAKRISTO 106 WAUWAWA KWA RISASI NA KUCHINJWA NIGERIA
Tokea 2014 ianze, zaidi ya Wakristo 130 wameripotiwa kuuwawa. ©CBN News
Unafanayeje, watu wanapozingira kijiji (mtaa) chenu na kuanza kuvamia kaya moja baada ya nyingine, kupiga risasi na kuchinja kooni wanaume wote wa kijiji chako? Unafanyeje pale ambapo kama wewe ni mwanamke na ukitaka kumtetea mwanaume yeyote, kuanzia mume, mtoto na hata mjukuu, basi nawe unauwawa? Na kisa cha haya yote ni kutakana na imani yako, kwamba tu umechagua kuwa Mkristo.
Jumapili, 16 Februari 2014
USIOE AU KUOLEWA KWASABABU KAMA HIZI
Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa huduma ya Voice of Hope Ministries (VHM)
USIOE AU KUOLEWA KWASABABU YA KUMSAIDIA MTU FULANI AU KUMUONEA HURUMA
1. Kuoa au Kuolewa na Mtu kwasababu ya Kumuonea Huruma.
• Kuoa au kuolewa na mtu kwa sababu ya kumuonea huruma ni moja kati ya sababu zisizo sahihi. Na inaonekana kuwa ni sababu moja ya kijinga pia.
•Ndoa zianazo oana kwa misingi ya kumsaidia mtu au kumwonea mtu huruma huwa hazina maisha.
2. Huruma ya Kujiona kuwa ni wewe Ndio Unawajibika.
Jumamosi, 15 Februari 2014
UKUMBI WA PTA WARINDIMA KWA MAOMBEZI YALIYOFANYWA NA WAPENTEKOSTE KWA TAIFA
Siku ya jana ndani ya ukumbi wa PTA uliopo ndani ya viwanja vya maonyesho vya mwalimu JK Nyerere almaarufu kama Sabasaba kulifanyika maombi maalumu kwa Taifa yakiongozwa na umoja wa makanisa ya Kipentekoste nchini. Katika maombi hayo yaliyohudhuriwa na waumini lukuki sambamba na wachungaji wao ilishuhudia askofu Zachary Kakobe pamoja na Josephat Gwajima wakiongoza maelfu ya waumini waliofika ukumbini hapo katika kuhubiri neno la Mungu kwa ufupi kisha kuingia katika maombi ambayo yaliandaliwa vyema na umoja huo.
Jumanne, 11 Februari 2014
KUJUA KAMA JINA LAKO LIMEANDIKWA KITABU CHA UZIMA NI SHILINGI ELFU 20,000 TU
Nabii mchungaji Thomas Wahome. © courtesy
Ikiwa takribani miezi miwili tangu kujulikana kwa huduma ya mtume Lesego wa Afrika ya kusini kuwaagiza waumini wake kula manyasi sambamba na kuwafanyia maombi akiwa amewakanyaga migongoni, mambo bado yanaendelea kwa watumishi wa Mungu waliopo Afrika kushangaza ulimwengu kupitia huduma zao.
Mchungaji Josephat Gwajima
Ufufuo na Uzima,Tanganyika Packers Kawe Utangulizi ZABURI 18
Mungu aliwaumba watu na akawaagiza wazae na kuongezeka juu ya uso wa nchi lakini wakapatikana watu waliokwenda kinyume na amri hiyo ya Mungu na kufanya kinyume, wao wakasema watakaa mahali pamoja ili wasitawanyike usoni pa nchi. Unaanza kujifunza kumbe wanaweza wakapatikana watu wakaenda kinyume na mambo yale ambayo Mungu amesema juu ya maisha yako, Mungu anataka ubarikiwe, uwe na afya njema na ufanikiwe lakini wapo waganga na wachawi na wanadamu ambao wanaweza kuja kinyume na makusudi ya Mungu katika maisha yako.
SOMO : HAKIMU ALIYE TOFAUTI NA MAHAKIMU WOTE
Askofu Zachary Kakobe. |
Siku ya kufa kwa mwanadamu fulani, ni siku ya mwisho wa dunia kwa mtu huyo. Iko siku ya mwisho wa dunia kwa watu wote ulimwenguni, hata hivyo, iko siku ya mwisho wa dunia kwa mtu mmoja mmoja binafsi, nayo ni siku ya kufa kwake. Nani kati yetu anayeijua siku ya kufa kwake? Hakuna hata mmoja aijuaye. Siku tusiyoidhani, ndipo tunapokutana na kifo. Kifo siyo lazima kije kwa mtu baada ya kuugua kwa muda mrefu. Hakuna kanuni. Tunaweza tukapatwa na ajali, tunaweza tukalala usiku, halafu ndiyo ikawa mwisho wetu n.k. Kifo hakina uzee au ujana au utoto. Watoto wengine wamefariki na kuwaacha babu zao wakiwa hai! Ndiyo maana Biblia inasema katika MHUBIRI 9:12, “Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla”.
YESU NI NANI?
Yesu wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako hapa duniani na ya milele yanaguswa na jibu lako kwa swali hili?
Nani, kwa maoni yako, ni...
Mtu wa ajabu kupita watu wote katika nyakati zote?
Nani aliyejitokeza kuwa mtu mashuhuri kwa vipindi vyote?
Kiongozi mkuu?
Mwalimu mkuu?
Mtu aliyefanya matendo mema kwa wanadamu kupita mwingine?
Mtu aliyeishi maisha matakatifu kuliko yeyote aliyewahi kuishi?

Jumapili, 9 Februari 2014
HOJA YA ASKOFU GAMANYWA: FALSAFA YA UMILIKAJI KWA MUJIBU WA BIBLIA (4)
Rais wa WAPO Mission International, Aksofu Sylvester Gamanywa
Katika makala yaliyopita tulisoma habari Utoaji unaotambulika; na Mtindo wa utoaji wa “Injili ya utajirisho”. Kisha tukajifunza juu ya Tofuati kati ya “Injili ya utajirisho” na“Falsafa ya kumilikisha” kwa mujibu wa Biblia. Leo tunaendelea kuchambua katika maeneo haya haya ukiwa ni mwendelezo wa somo lililopita:
Jumamosi, 8 Februari 2014
GLORIOUS YAANZA USIKU WA MATUMAINI KWA KISHINDO
Usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa 92 Hotel ama Shalom Tabernacle church kulifanyika mkesha wa kwanza wa aina yake ufahamikao kama Motivational Friday Night chini ya kundi matata la injili nchini la Glorious Worship Team, ambao wamerejea tena kuwakusanya wapendwa na marafiki zao kila Ijumaa kuanzia jana na ijumaa zote zinazokuja kwahiyo mdau usikose kila siku za ijumaa ndani ya Hotel 92 karibu na Sansiro Shekilango jijini Dar es salaam.
Tazama picha japo kwa uchahe, GK itakupasha kilichojiri kwa upana ikiwemo video za tukio hilo
Barikyiz na Paul Clement
Tazama picha japo kwa uchahe, GK itakupasha kilichojiri kwa upana ikiwemo video za tukio hilo
Barikyiz na Paul Clement
Jumatano, 5 Februari 2014
KWA TAARIFA YAKO : MALIZIA TAARIFA ZA MWIMBAJI INJILI ALIYENUSURIKA KUWA MSUKULE
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GKikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO Mchungaji Nicodem anasema alikuwa hana huruma na wachawi hata kidogo na mpaka sasa bado anapambana nao, hali hiyo ilimfanya ampe siku thelasini (30) Baba yake mzazi aokoke la sivyo angekufa. lkn wakati huo pamoja na baba yake kuwa ni mchawi alikuwa pia ni mtumishi wa kanisa,. KWA TAARIFA YAKO Baba yake alianza kuumwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo ilipofika siku ya 28 alikuwa mahututi na ndipo alipopigiwa simu na kwenda kumuona mgonjwa huku akiwa amebeba soda. (Kama hujasoma sehemu zilizopita BONYEZA HAPA)
KWA TAARIFA YAKO Alipofika sehemu ambapo amelazwa baba yake akaaanza kumuita Baba Baba unaendeleaje Baba ndipo Baba yake akauliza wewe ni nani? akajibu mimi ni Nico nimekuja kukuona unaendeleaje lkn pia nilikuwa nakushauri ungempokea Yesu anaponya. KWA TAARIFA YAKO Baba yake alimjibu "Shut up Ng'ombe kasoro mkia mtoto mchawi wewe umekuja kunimaliza mimi hadi hospital toka nje" Madactari wakashangaa mgonjwa alikuwa amezidiwa anaongea wakaja na kumtoa Mch Nico naye akakubali kutoka nje akachukua soda aliyompelekea mgonjwa huku akisema wembe ni ule ule.
KWA TAARIFA YAKO Baba yake alifariki dunia kama alivyosema mchungaji Nico kwamba asipo okoka kwa mda wa siku 30 alizotoa basi atakufa na kweli Baba yake alikufa.KWA TAARIFA YAKOMchungaji Mwangila anasema mapambano hayakuishia hapo kwani walikuwa wamebaki makonkodi wengine watatu ambao ni Mme wa Shangazi yake, Baba yake mkubwa na Babu yake Mdogo ambao hao walipanga kumuangamiza.
KWA TAARIFA YAKO Mch Nico anasema alipewa taharifa ya msiba kijini ukiwa ni msiba wa Babu yake mwingine ambaye alikuwa pia mchawi akiitwa mzee John na aliamua kununua blangeti la kwenda kuzikia na alipofika kijijini hao wazee watatu waliuobaki walikuwa wamepanga hila ya kutaka kumuangamiza. KWA TAARIFA YAKO walipanga kumwangamiza kwa kutumia nyama pindi atakapo kula imkabe koo na kummaliza kabisa. Alipofika hapo walimpokea kwa furaha mpaka akashangaa na kumkaribisha ndani na hapo pia walikuwa wametoa maagizo kwamba Nico akifika apakuliwe nyama ale kablda ya watu wengine.
KWA TAARIFA YAKO mara baada ya kukaa ndani wakampakulia nyama na kumpelekea lkn kabda ajaanza kula akasikia sauti inamwambia kuwa "Nico hizo nyama ulizopewa sio nyama hayo ni mabomu kwemye ukoo wenu kuna uchawi unaitwa uchawi wa manyambuda , manamuua mtu akiwa anatembea au anaota moto au alikuwa analima mnamkuta amekufa, kwahiyo wameweka hiyo ukila kituli kimoja tu akitapita shingoni kitakukaba kwenye koo na wanataka wakuzalilishe mbele ya umati wa watu hapa msibani" KWA TAARIFA YAKO akaambiwa tena "Tazama mkono wako wa kulia " akawaona Babu Mdogo, Mme wa Shangazi pamoja na Baba Mkubwa wakiwa wamekaa pembeni huku mikono yao wakiwa wameshikilia shingo ili alakapo kula waminye sehemu ya koo na kumuua.
KWA TAARIFA YAKO Hapo ndipo mchungaji Nico aliposema hizi nyama abakishi mtu nakula sahani yote namaliza na naendakuongeza tena na hata kama akione kana mroho atahakikisha abakishi kitu.KWA TAARIFA YAKO akaanza kuomba kwa kunyunyuzia Damu ya Yesu na kuzitakasa pamoja na kufutilia mbali manuizo yote yaliyowekwa kwenye nyama. Mara baada ya kumaliza kuomba akaanza kula nyama na kumaliza sahani na KWA TAARIFA YAKO alirudia mara nne huku wale wazee wakibaki kumtolea macho hadi anamaliza huku yeye akijisemea moyoni mwake "Leo amli kitu nahakikisha namaliza nyama zote"
KWA TAARIFA YAKO alikula na kumaliza salama bila kudhurika na lolote hali ambayo imemfanya kuogopwa na kuheshimiwa katika ukoo wao huku wakisema huyu mtoto ni hatari sana sijui ameutoa wapi uchawi huu kwani kwenye ukoo hakuna mtu alikuwa na uchawi namna hii. KWA TAARIFA YAKO Mchungaji Nicodem Mwahangila anasema uchawi wake ameutoa kwa Yesu na kamwe hawezi kumwacha na mapambano dhidi ya wachawi popote pale atakapo kanyaga yanaendelea kama kawaida.
KWA TAARIFA YAKO Huyo ndiye Mchungaji Nicodem Mwahangila ambaye GK imekuelezea kwa sehemu maisha yake na jinsi Mungu anavyomtumia katika maombi ya vita. Pia Mchungaji Nico ni muimbaji na kwasasa ametoa toleo la pili linaitwa Hakuna Kubebwa, Zaidi wasiliana nae kwa 0756 27 30 49
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo vinginevyo tukutane wiki ijayoo

Jumanne, 4 Februari 2014
ASKOFU KAKOBE : TOFAUTI YA KUPUNGA PEPO NA KUTOA PEPO
Jumapili, 2 Februari 2014
HARUSI YA KANA (Wedding in Cana of Galilee) *sehemu ya nne*
Na Mtumishi Gasper Madumla
Shalom...
Bwana Yesu asifiwe...
Nasema;
Haleluya...,Haleluya...
Fundisho hili sio la kukosa,maana lipo kusudi kwako wewe usomaye ujumbe huu.
Ni kweli umeshawahi kusoma mafundisho mengi sehemu mbali mbali,lakini mimi nakuhakikishia kabisa,kwamba utapokea mambo makubwa sana usomapo fundisho hili mahali hapa,na Bwana mwenyewe anakwenda kukuhudumia sasa.

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)