Alhamisi, 7 Novemba 2013

MWANAMAMA WA KIBAO CHA "CALVARY" SPIRIT OF PRAISE APATA MTOTO WA KIKE


Zaza akiimba kibao cha Calvary wakati wa onyesho la Spirit of Praise mwezi August mwaka huu.
Mwanamama Zanele Mokheti Mosike au mwite Zaza wa kundi la Spirit of Praise amefanikiwa kujifungua mtoto wa kike hapo jana, mwanamama huyo anayetamba kwasasa na pambio la Calvary linalopatikana katika toleo la nne la Spirit ametangaza kupata mtoto wa kike hapo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook. Mara ya mwisho kuonekana jukwaani ilikuwa mwezi wa tisa mwaka huu kisha akaamua kupumzika kutokana na hali aliyokuwa nayo.

Jumatatu, 4 Novemba 2013

NATAKA NIPATE KUONA* sehemu ya mwisho* Marko 10:51


Mtumishi Gasper Madumla.

Bwana Yesu asifiwe...
Jina la Bwana lisifiwe sana...
Haleluya...

"Yesu akamjibu,akamwambia,Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia,Mwalimu wangu,NATAKA NIPATE KUONA" Marko 10:51

Ni maombi yangu kwako wewe mpendwa usomaye ujumbe huu,kwamba Mungu wa mbinguni,Baba yetu,Jehova akusaidie upate kuona kiroho.

NINAMWAMINIJE TENA MTU ALIYENITOSA WAKATI WA TAABU YANGU?



Na Pastor Carlos Kirimbai.
MIT. 25:19 SUV

Kumtumaini asiye mwaminifu wakati wa taabu Ni kama jino lililovunjika, au mguu ulioteguka.

Ngumu sana.

Yesu alisema haya maneno kwa wanafunzi wake waliyodumu pamoja naye hata katika magumu Yake.

LK. 22:28-30 SUV

Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.

BINGWA WA KUFUNGA WANAFUNZI MIMBA WASIJIFUNGUE AKIMBILIA KWA YESU

Kuna habari ama stori zimewahi kuvuma katika mikoa mbalimbali kwamba kuna watu wanaofanya kazi za uganga wanaweza kufunga hata mimba ya mtu asijifungue mpaka atakapo maliza shida yake ndipo ajifungue, mfano ni wanafunzi ambao yawezekana wanapata mimba wakingali masomoni hivyo huenda kwa waganga hao kutaka kufungwa mpaka wamalize shule, jambo hili kisayansi haiwezekani hata kiduchu lakini katika ulimwengu wa kishirikina haya mambo wanayo. Nisikuchoshe soma ushuhuda hapo chini wa mzee huyu aliyekuwa bingwa wa kufunga wanafunzi mimba mkoani Kigoma.


Mzee huyu akiwa na mke wake katika madhabahu ya Ufufuo na uzima kigoma alianza kuwa mganga wa kienyeji tangu mwaka 1972 pia aliwahi kuwa mwalimu mkuu wa shule ya sekondri Ujiji Kigoma. Baadhi ya kazi alizokuwa akizifanya ni kufunga mimba za wanafunzi ambao hawakuwa tayari kujifungua kwa muda huo, amesema kama mtu akimwambia anashida ya kutoa mimba, alikataa kutoa mimba bali aliweza kuizuia wala isiweze kukua mpaka wakati binti atakapomaliza masomo yake au atakapohitaji kujifungua.

Jumamosi, 2 Novemba 2013

UWEZEKANO WA KUMSALITI YESU

Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA
SOMO: UWEZEKANO WA KUMSALITI YESU

Leo, tunajifunza Biblia kutoka MATHAYO 26:1-30. Katika mistari hii, pamoja na mambo mengine, tunajifunza “UWEZEKANO WA KUMSALITI YESU”. Tutayagawa mafundisho tunayoyapata katika mistari hii katika vipengele tisa:-

(1) MWISHO WA UTUMISHI WA MTUMISHI WA MUNGU (MST 1-2)

(2) MAADUI WAKUBWA WA YESU (MST 3-5)

(3) KUWEKWA TAYARI KWA MAZIKO KWA KKUMWAGIWA MARHAMU (MST 6-13)

(4) SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA (MST 14-16)

UKOMBOZI KILIMANJARO HAUKWEPEKI

Ni kama vile dozi ya injili imeshauriwa na Daktari Bingwa, maana baada ya uwanja wa mashujaa jijini Moshi mkoa wa Kilimanjaro kuhitimika kwa mkutano mkubwa wa kanisa la Utukufu wa Yesu, sasa viwanja hivyo vinapumua kwa siku chache tu kabla ya watumishi wengine kuendelea na ratiba ua injili.
Zamu hii wakati Ufufuo na Uzima wakiwa kwenye jengo ambalo watakuwa wakilitumia kama kanisa la mkoani humo, mtumishi wa Mungu kutoka Sweden, Mwinjilisti Johannes Amritzer atapiga kambi kwa takriban siku tano, kutakuwa na sherehe ya miujiza.



Pamoja na kuhubiri matendo makuu ya Mungu, waimbaji kadha wa kadha watakuwepo wakiwemo Anne Annie, Kilimanjaro Gospel Choir, na wengineo wengi. Kupanga kukosa ni sawa na kutoroka usipate uponyaji wako.

Jumatano, 30 Oktoba 2013

DHIKI KUBWA



Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

Somo: Dhiki kubwa

Tunajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele saba.

( i ). Dhiki tofauti na zote

( ii ). Muda wa dhiki kubwa

( iii ). Majina yanayotumika kuzungumzia dhiki kubwa

( iv ) Watakaohusika kuileta dhiki kubwa

( v ). Makusudi ya dhiki kubwa

( vi ) Hali itakavyokuwa wakati wa dhiki kubwa

( vii ). Jinsi ya kuikwepa dhiki kubwa

( I ). DHIKI TOFAUTI NA ZOTE

Wanadamu hapa duniani, wanapitishwa katika dhiki za namna namna. Wanapitishwa katika mateso ya namna namna. Wengine wanapitishwa katika hali nzito ya njaa nchi nzima hali inakuwa mbaya. Nchi ambazo zimewahi kushuhudia njaa kali kama Ethiopia na Somaria, watu watakondeana na kubaki mbavu kabisa.

BARAZA LA MAKANISA KENYA LAUNGA MKONO VIONGOZI WA MAKANISA KUKABIDHIWA BUNDUKI KUJILINDA


Katibu mkuu wa Baraza la makanisa nchini Kenya NCCK mchungaji Peter Karanja. ©Dailynation.
Watu mbalimbali nchini Kenya wakiwemo waumini wa dini ya Kikristo wamepinga wazo lililotolewa na viongozi wa dini hiyo kwamba wakabidhiwe bunduki aina ya AK47 ili kupambana na waumini bandia wa dini ya kiislam nchini humo ambao wamesababisha kifo cha mchungaji pamoja na kuchoma kanisa huko mkoani Mombasa nchini Kenya.

KWA TAARIFA YAKO : ALIYEIMBA "MFALME DAUDI" THE BIG NOVEMBER CRUSADE UNAJUA ALIKO?

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


KWA TAARIFA YAKO hii leo mdau wetu ni kuhusiana na mwimbaji aliyewahi kuwika jijini Dar es salaam kutokana na uimbaji na uhamasishaji wake katika kumtukuza Mungu, huyu si mwingine bali ni Allen Kinsalla Lopez mwimbaji huyu alipachikwa jina la "Mfalme Daudi" kutokana na ghani yake ama rap yake ya "Mfalme Daudi, mfalme Daudi alicheza x2 aliicheza nguo zote zikaanguka, tuchezetuchezze kwa BWANA YESU tucheze, turukee turuke kwa BWANA YESU turukee……"rap hii ilipata umaarufu sana wakati wa mikutano ya "The Big November Crusade" iliyokuwa ikifanyika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.

Mwimbaji huyu bwana Allen Kinsalla ambaye pia alikuwa ni mwimbaji wa kwaya ya Uinjilisti Sayuni Kinondoni Lutheran, yeye pamoja na kundi la kusifu na kuabudu ama stage band ilivyozoeleka katika mkutano huo walikuwa wakipenda sana kuimba pambio "Yale alotenda ndani yangu" na mapambio mengine ambayo yalikuwa yakiwakaribisha katika uwepo wa Mungu, mamia ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake ambao walikuwa wakifika katika mkutano huo.




Kwasasa mwimbaji huyo mwenye asili ya Congo Kinshasa anaishi nchini Marekani pamoja na familia yake kwa maana ya mkewe na watoto wawili. Mwimbaji huyu alikuwa kipenzi cha wanafunzi wa Ushirika wa kikristo wa wanafunzi Tanzania(UKWATA) mkoa wa Dar es salaam na Pwani wakati ambao kwaya ya Sayuni ilikuwa ikialikwa kila mwaka kwenye makambi ya pasaka, matamasha, joint mass pamoja na sherehe mbalimbali za wanafunzi hao wanapohitimu masomo yao(Graduation za UKWATA).

BAADA YA MUNGU KUJIDHIHIRISHA KILIMANJARO, UFUFUO WAPATA JENGO MAELFU WAHAMIA


Jengo linavyoonekana kwa nje.

Baada ya kumalizika kwa mkutano mkubwa wa injili viwanja vya mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, mmoja kati ya watu waliohudhuria katika mkutano huo ametoa jengo lake kubwa ili litumiwe na kanisa la Ufufuo na uzima kwaajili ya huduma mbalimbali zikiwemo ibada.

Jumatatu, 28 Oktoba 2013

unabii; TB JOSHUA ATOA TAHADHARI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI,"KUNA RAIS ATATEKWA NA KUTAKUWA NA MILIPUKO YA MABOMU KWENYE CLUB HIZI"!!!

Yule Mchungaji Maarufu kutoka Nigeria Ambae hutabiri mambo mbalimbali na kweli yakatokea TB Joshua jumapili hii ametoa utabiri mpya ambao unahusisha Africa Mashariki ...ameonyeshwa rais mmoja Africa Mashariki atatekwa na ameonyeshwa watu wakiwa club wanacheza nakisha wanalipukiwa na nchi iyo ni jirani na Kenya,

Jumamosi, 26 Oktoba 2013

HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI

Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SIKU YA KUICHAMBUA BIBLIA

SOMO: HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI
L
eo, tunamaliza kutafakari SURA YA 14 ya Kitabu cha YOHANA katika Biblia zetu. Tunachukua muda wa Siku ya leo ya Kuichambua Biblia, kujifunza YOHANA 14:13-31. Katika mistari hii, pamoja na mambo mengine, tutajifunza kuhusu, “HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI“. Tutayagawa mafundisho yote tunayoyapta katika mistari hii, katika vipengele tisa:

(1) KUOMBA KWA JINA LA YESU (MST. 13-14);

(2) HAKIKA YA KUJIBIWA MAOMBI (MST. 13-14);

(3) ALAMA YA KUMPENDA YESU (MST. 15, 21, 23-24);

(4) MSAIDIZI MWINGINE (MST. 16-27, 25-26);

(5) SITAWAACHA NINYI YATIMA (MST. 18-20);

NATAKA NIPATE KUONA *sehemu ya pili*

CHANZO;GOSPLE KITAA.

Mtumishi Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe...
Nakusalimu mpendwa katika Jina kuu la uweza la Yesu Kristo,
Nikikuambia ;

Jina la BWANA lipewe sifa....

Dhima kubwa ya fundisho hili ni kupata kona kiroho.
Maana hakuna jambo lililo kubwa kama kuona kiroho. Yeye mwenye kuona kiroho ni mtu wapekee sana,maana hata maombi yake huwa ni yakipekee.

Leo tunajifunza kiundani kwa habari ya Bartimayo ambaye alifanikiwa kupata kuona. Nasi tunahitaji tupate kuona.

Nampenda sana huyu Bartmayo kipofu.
Yeye alijua jambo moja tu,;

KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA YA HAR-MAGEDONI

Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO: KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI

Tuliangalia katika masomo yaliyopita kwamba, Dhiki kubwa au Dhiki kuu, itachukua kipindi cha miaka saba ( 7 ). Katika kipindi hiki pia, watakatifu walionyakuliwa wakati wa kunyakuliwa kwa kanisa, watakuwa katika kipindi cha kupewa taji na kufanyiwa karamu ya harusi ya MwanaKondoo. Ni makusudi ya somo letu la leo kujifunza tukio litakalofuata mwisho wa miaka hii saba, Kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili duniani na Vita vya Har-Magedoni. Tutaligawa somo letu la leo katika vipengele vitano:-

( 1 ). KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI.

( 2 ). TOFAUTI YA KUJA KWA YESU WAKATI WA KUNYAKULIWA KWA KANISA NA KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI

( 3 ). MAKUSUDI YA KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI

( 4 ). TAIFA LA ISRAELI WAKATI WA KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.

( 5 ). VITA VYA HAR-MAGEDONI NA KUFUNGWA KWA SHETANI MIAKA ELFU MOJA.

( 1 ). KUJA KWA YESU MARA YA PILI DUNIANI.

Yesu Kristo, mara ya kwanza, alikuja hapa duniani katika udhaifu na unyonge kwa kuzaliwa na Mariamu na kulazwa katika Hori kulia ng’ombe. Kwa Waisraeli ambao hawakujua maandiko vema, hawakutambua kwamba Kristo Kristo ni Yesu kutokana na mazingira yake ya umaskini na unyonge ( LUKA 9:58; 2 WAKORINTHO 8:9 ). Walidhani wakati ule wa kwanza angekuja kama Mfalme na kushindwa kafahamu kwamba wakati wa kuja kama Mfalme, ilikuwa wakati wa kuja kwake MARA YA PILI duniani. Wakati wa kuja kwa Yesu mara ya pili, atakuja katika mazingira tofauti kabisa na pale mwanzoni. Atakuja na hali zifuatazo:-

MKUTANO MKUBWA WA INJILI UNAOENDELEA MJINI MOSHI. SOMO: LAANA ZA FAMILIA Na Mchungaji Kiongozi: Josephat Gwajima


Mch.Kiongozi Josephat Gwajima.
Kuna familia zinaandamwa na matatizo mbalimbali, mfano. matatizo ya kutokuolewa,umasikini au matatizo mengine yanayotokana na laana za familia. Mchungaji Kiongozi alihaidi kuvunja matatizo yote ya kifamilia yanayoletwa na familia,na kusema kuwa leo kuna mambo ambayo anataka kuusemea ukweli.
kuna familia ambazo zinakuwa zipo chini ya laana fulani na hata mtu akipenya anapenya kwa taabu sana.
Sasa tutaangalia siri iliyopo nyuma yake halafu utafunguliwa katika Jina la yesu.
Tukiangalia maandiko

Mwanzo 9:18-25..
18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
19 Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.
20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

SHUHUDA, MKUTANO WA INJILI MOSHI WALIOCHUKULIIWA MISUKULE WA RUDI,alikuwa makaburini Tanga,mwingine alikuwa Singida kwenyye mashamba ya mpunga.



Matendo makuu ya Mungu aliyoyafanya Arusha, imemfanya leo MIRRIUM mkazi wa Arusha kufika katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi kushuhudia Mungu alivyo mponya.Mirium alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo kuvimba, na uvimbe tumboni. Alishuhudia kuwa mara baada ya kuhudhuria mkutano huko Arusha uliokuwa katika viwanja vya relini, alipokea uponyaji wake papo hapo. Binti huyu hakuishia hapo aliamua kwenda katika hospitali ya MOI kuhakikisha muujiza Mungu aliomtendea. Huku akiwa na uso wa furaha, alishuhudia mbele ya madhabahu kuwa mara baada ya kwenda kufanya uchunguzi hospitalini madaktari walithibitisha muujiza wake maana amekuta moyo wake umepona na uko vizuri na uvimbe umetoweka kabisa.


Hakika sauti ya "njoo kwa jina la Yesu" inarudisha watu kutoka mateka,Isaya 42:22... Huyu anaitwa DORIS ana umri wa miaka 13, alichukuliwa mateka na kuwekwa uvunguni mwa kitanda. Leo binti huyu kaisikia sauti ya njoo kaifuatana nakujikuta yuko katika kundi la watu wengi.Yesu ni yuleyule jana na leo na hata milele.




Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima akihoji binti aliyepatwa na muujiza wake katika maombi, Yesu alisema Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake, EUGENIA PHILIPO mkazi wa mjin moshi, mwenye umri wa miaka 22, alichukuliwa na mama yake mdogo na kuwekwa katika zizi la ng’ombe. Huko alikuwa akifanya kazi ya kulisha ng’ombe na kukamua maziwa, huku chakula chake kikiwa ni nyama za watu na kunywa damu.

kama vile haikutosha mama wa binti huyu pia alikuwa akimtumikisha kwa njia ya kichawi kwenda kukamua maziwa ya ng’ombe kwa watu. Aliendelea kushuhudia kuwa ng’ombe wa majirani walikuwa hawatoi maziwa kwa sababu ya kuibiwa kichawi na binti huyu. Yule mtenda miujiza ambaye alikirimiwa Jina lipitalo majina yote YESU KRISTO leo kamtoa katika utumwa wa shetani na kumuweka huru.

Alhamisi, 24 Oktoba 2013

UKOO WA MALKIA UINGEREZA WATAKIWA KUMLEA MTOTO AMJUE YESU, ANGALIA PICHA ZA UBATIZO


Askofu mkuu wa Canterbury kanisa Anglican duniani Justin Welby amewataka wazazi na wadhamini wa mtoto Prince George Alexander Louis kuhakikisha mtoto huyo anamjua Yesu ninani katika maisha yake. Askofu Welby ameyasema hayo wakati akimbatiza mtoto wa kwanza wa mjukuu wa malikia Elizabeth wa Uingereza, Prince William na mkewe Kate Middleton katika ibada fupi iliyohusisha familia pamoja na wageni wao 22 na kufanyika katika kanisa la kifalme ndani ya jengo la Mtakatifu James jijini London.

Wakati wa ibada hiyo baba mdogo wa mtoto huyo Prince Harry alisoma neno kutoka kitabu cha Yohana 15:1-5 ukizungumzia suala la mzabibu na matawi huku mama mdogo wa George, Pippa Middleton kwa upande wake alisoma neno kutoka kitabu cha Luka 18:15-17 ukizungumzia Yesu aliposema waacheni watoto wadogo waje kwangu. Katika ubatizo huo uliohudhuriwa na malkia pamoja na mumewe Prince Philip jumla ya wadhamini ama walezi wa mtoto wapatao saba walichaguliwa wakiwemo kutoka ukoo wa ufalme, marafiki wa karibu na Prince William pamoja na rafiki wa karibu sana na marehemu Princess Diana aitwaye Julia Samuel.

Askofu Welby alitumia maji ya mto Yordani katika kumbatiza prince George maji ambayo yamekuwepo katika kanisa hilo lenye historia ya ukoo wa kifalme toka mwaka 1894. Kwa mujibu wa Prince William amesema mwanae hajasumbua hata kidogo ikiwa ndio siku yake ya kwanza hadharani toka azaliwe, ambapo imeelezwa mtoto huyo kuonekana mwenye furaha na tabasamu toka awasili na kutoka kanisani hapo, huku muonekano wake ukiwa kama baba yake alivyokuwa katika umri kama huo.



Kate Middleton akiingia na mwanae.


Prince William akiwa mwenye furaha na mtoto wake Prince George mwenye miezi mitatu.


Wazazi wenye furaha na mtoto wao ambaye yupo katika mstari wa tatu katika urithi wa kiti cha ufalme Uingereza.

ONA NAMNA MALAIKA WALIVYOMUOKOA MWIMBAJI NYOTA KWENYE AJALI


Gari likiwa limepinduka bondeni.

Mwimbaji anayetamba na wimbo wa "Zawadi gani nitamtolea BWANA" ambaye pia ni mtume akichunga kanisa jijini Dar es Salaam John Komanya amepata ajali mbaya juzi mchana maeneo karibu na daraja la Mto Wami akiwa njiani kuelekea mkoani Arusha kukutana na viongozi wanaohudumu na mwalimu Christopher Mwakasege, kwa ajili ya mkutano wa injili ambao utakuwa na lengo la kuombea taifa kwa siku nne mwezi Disemba.

Kama una Mashaka na Huamini huduma ya mtumishi fulani…EPUKA KUWASEMA VIBAYA,TUMIA HEKIMA


KAMA UNA MASHAKA NA HUAMINI HUDUMA YA MTUMISHI FULANI, USIFUNGUE MDOMO KUMSEMA AU KUWASHAWISHI NA WENGINE WAWE NA CHUKI NAYE; KWA KUFANYA VILE, HATA KAMA UNACHOKISEMA NI SAHIHI, LAKINI TAYARI HAUJAKIFANYA KWA KANUNI ZA KIMUNGU, CHUKI YAKO NI SAWA NA UUAJI!
NJIA RAHISI YA KUSHUGHULIKA NA HUYO AMBAYE WEWE UNA MASHAKA NA HUDUMA YAKE AU HUAMINI KWAMBA NI MTUMISHI WA MUNGU, FANYA HAYA YAFUATAYO:

miujiza,WALIOKUWA VIWETE ZAIDI YA SABA WATEMBEA BAADA YA MAOMBEZI MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA - MOSHI NA Mch. Josephat Gwajima

WATU ZAIDI YA SABA AMBAO WALIKUWA NI WALEMAVU KABISA WA MIGUU, HATIMAYE WAWEZA KUTEMBEA BAADA YA KUOMBEWA NA MCH.KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI UNAOENDELEA MJINI MOSHI, MATUKIO HAYA NI YA SIKU YA JUMATANO TAREHE 23.10.2013

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kutoka Kawe Jijini Dar es Salaam akiwaombea maelfu ya waamini katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi, maelfu ya wakazi wa mjini Moshi walikusanyika kwa ajili ya kusikiliza Neno la Mungu,Kuombewa na kuwekwa huru kutoka katika vifungo vya shetani.




Mchungaji kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima wa kwanza kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na walioponywa ulemavu wa miguu na kushoto kwake ni Petronila anafuatiwa na Mama Ruckless na wa