Jumamosi, 27 Mei 2017

YESU ANAKUPENDA





Na Mtumishi Oscar Samba.
Wanadamu wanaweza kukuchukia, kukutenga, kukubagua, kukudharau na hata kukunyanyapaa ila huyu YESU hawezi kukutenda hayo badala yake ni wa Upendo daima.

 

Hajui kumchukiwa mtu, hata kama ni Kahaba, Mlevi, Mwizi, Mtukanaji, jamii inamuona kama Kichaa ama aliyechanganyikiwa na Maisha ama kurukwa na Akili.

Yesu bado ni wa upendo kwake na anampenda zaidi, Yesu huyu anampenda hata yule anayejihukumu kwa kuwa ametenda dambi nyingi sana kwa hiyo hasitaili msamaha wa Mungu. Hapana!  Kila mtu alitenda dhambi tena na kupungukiwa na Utukufu wa Mungu ila Yesu alikufa kwa ajli yake na maneno hayo siyo ya kwangu bali ni ya Bibilia, kitabu ambacho yamkini uliwai kukisikia ama ndo unakisikia leo ila ni kitabu chenye maneno mazuri ya Mwenyezi Mungu yaletayo uponyaji na kama ujakisoma usisite kukisoma maana hakibagui dini, kabila ama rangi wala umri ama adhi fulani.

 

Ukisoma katika Kitabu chenye jina la INJILI YA YOHANA sura ile 3 mstari wa 16, utakutana na ujumbe huu. (Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.)

 

Upendo huu ni kwa ajili yako ndugu yangu, wewe mwenyewe ni shahidi ya kwamba hata ule unayempenda ama anayekwambia kuwa anakupenda hawezi kukufia yaani kuwa tayari kufa kwa ajili yako ila huyu Yesu alitufia na hii ni matokeo ya upendo.

 

Kulikuwa na kisa kimoja cha watu waliokuwa ni wapenzi na walionekana kupenda haswa kwa jinsi ya mwili, ila wakiwa pamoja na wakiahidiana kutokuachana na kuwa radhi kufa pamoja, gafula kulitokea watu waliosadikika kuwa ni wauaji ama waporaji. Kilichofwata ni kila mtu kukimbilia njia yake wala hakuna aliyemkumbuka mwenzake.

Kisa kingine kilimuhusisha mama aliyekuwa akinyonyesha ama mwenye mtoto mdogo na ilipotokea ajali alikimbi na kumsahau mwanaye na mara baada ya muda kitambo ndiposa kumbukumbu ya mwanaye ikamjia.

 

Yesu huyu wakati anakamtwa hakufanya hivyo bali alitukumbuka hata katika nyakati ngumu kama hizi. Ni wangu wito majira haya kukubali upendo huu wa ajabu wa Yesu Kristo ili akuokowe na kukusaidia kutoka katika adha ulizo nazo. Na ukiokoka pia utakuwa na uwakika wa safari yako ama utakakokwenda mara baada ya kifo.

Natumai hivi sasa upo tayari kuokoka ili Yesu awe Msaada wako sasa.

Kama ndio Fwatisha maneno haya kwa Imani, Sema BWANA YESU, NINAKIRI, YAKWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA WEWE NI MUNGU NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, INGIA SASA NDANI YANGU NA UNIOKOWE. AMENI.

Hongera kwa kuokoka natafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

MAWASILIANO: SIMU +255 759 859 287. WEB: www.mwanakondooinjili.blogspot.com

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni