Jumatatu, 29 Mei 2017

UHAKIKA BAADA YA KUFA.

Na Mtumishi Oscar Samba.

(MWANAKONDOO Ministry)

Ni jambo jema kuwa na uhakika wa maisha utakayo ishi ama sehemu utakayoenda mara baada ya kufa. Na uhakika huo unatokana na wewe jinsi ulivyo amua kuyaishi maisha unayoishi hivi sasa.
Maandiko yanasema wazi ya kwamba mara baada ya kufa ni hukumu, ikiwa na maana huwezi kutubu baada ya kufa ama hakuna atakayekuamulia mahali pakwenda mara baada ya kifo chako nikiwa na maana ya kwama hata ndugu zako wangekupenda na kukuombea kwa jinsi gani bado isingalikupa tiketi ya kubadilishiwa maisha ama sehemu upaswapo kwenda.

NINA MANTIKI YA KWAMBA, UWAMUZI WA UTAENDA WAPI UNAFANYIKA UNGALI HAPA DUNIANI NA SIO BAADA YA KUTOWEKA AMA KUNYAKULIWA. USIKUBALI KUDANGANYWA NA WIMBI LA UONGO WA MCHANA YA KWAMBA ETI UTAOKOKA MARA BAADA YA KUFA, AU UTATUBU UKIFA. HUO NI UWONGO WALA BIBILIA HAIJASADIFU JAMBO HILO.

Ni yangu rai kukutaka leo kuwamua mahali utakapo kwenda, Na kumbuka kuwa njia zipo mbili. 1. Kwanza ni ile ikupelekayo mbinguni na njia hiyo ni kumuamini Yesu. 2 Ni ile ikupelekayo Motoni ama kuzimu au Jehanamu ya moto. Na njia hiyo ni kutokumuamini Yesu. Kwa hiyo haijalishi unamatendo mazuri ama mema kiasi gani. Kama huja muamini huyu Yesu bado hutaweza kwenda Mbinguni. Kumbuka kisa cha Korinerio yule aliyekuwa Askari wa kiitalia kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume 10. Alikuwa mcha Mungu, aliwapa watu wengi sadaka ila Mungu hakuwa amemuandika kwenye kitabu cha wapasao kuipitia njia ya Haki, ndiposa akamtuma Petro ili amuongoze kumpokea huyu YESU.
Hatuendi mbinguni kwa matendo ya Sheria, wala wema tu, bali ni kwa kumuamini na kumkiri huyu Yesu. Uhakika huo tunaupata kenye kitabu kile cha Yohana mwanzoni mwa sura ya 14. Yesu anatuambia ya kwamba ameenda kutuandalia makazi ili alipo yeye nasi tuwepo hapo. Kwa hiyo kwa waliokoka uwakika upo.Na wewe fanya hima ili ukifa leo uende mbinguni.
Natumai hivi sasa upo tayari kuokoka ili Yesu awe Msaada wako sasa.
Kama ndio Fwatisha maneno haya kwa Imani, Sema BWANA YESU, NINAKIRI, YAKWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA WEWE NI MUNGU NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, INGIA SASA NDANI YANGU NA UNIOKOWE. AMENI.
Hongera kwa kuokoka natafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
MAWASILIANO: SIMU +255 759 859 287. WEB: www.mwanakondooinjili.blogspot.com

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni