Jumatatu, 29 Mei 2017

MKIMBILIE YESU.


Na Mtumishi Oscar Samba
 (MWANAKONDOO Ministry)
Haijalishi unakumbana na jambo gani, ama unaishi maisha ya aina gani,? Jamii uliyonayo inakuheshimu ama kukudharau. Ila ujumbe ambao Mungu amenipa siku ya leo ni huu; MKIMBILIYE YEYE.

Ukifika kwa Yesu kila kinachokusumbua kitakoma, magonjwa, mateso ya kimaisha, ugumu wa kiuchumi, ndoa kusumbua, taabu za kukataliwa na kutengwa na ndugu. Ama ni tabia za ukahaba, umalaya, wizi ulevi na hata ile ambayo hakuna nayeijua na nivigumu kumwambia mtu mwingine yeyote na mimi siwezi kuitaja hapa maana kimaadili sio vyema.
Katika hayo yote wewe mwendee YESU naye atakusaidia maana amesaidia wengi ikiwemo yule mwanamke aliyeonekana najisi kwa kunuka damu za mwezi na zilimtoka kwa muda wa miaka 12.

Fanya kama Zakayo ambaye alimkimbilia Yesu na kisha tabia ya kudhulumu watu kwa kuwatoza kodi zaidi ikakoma na hatimaye kufanya marejesho. Tunaupata ujumbe huu mtamu kwenye kitabu kile cha Luka 19:1-10, Utakutana na kisa hiki cha Zakayo ambaye alikuwa ni mtu mfupi wa kimo na aliposikia ya kwamba Yesu anapita katika njia ile alihakikisha ya kwamba anapanda juu ya mti wa mkuyu ili amuone na hatua hiyo ilikuwa ni ishara tosha ya kumkimbilia Yesu iliyomgarimu kupanda hata juu ya mti na mara baada ya hapo Yesu alimwambia hivi; (Zakayo, Shuka Upesi kwa maana leo imenipasa kushinda nyumbani kwako, Mstari wa 5.)

 Wokovu ulifika kwa mtu huyu, na wewe nakutaka kufanya kama Zakayo kwani nimekuletea Yesu na Yu katika njia anahitaji atakaye muhitaji ili ashinde naye nyumbani mwake ndaima yaani moyo mwake kwa kufanyika MUNGU ndani yake. Yesu akija kwako hakika hizo taabu za ugumu wa maisha, magonjwa, kukataliwa na kuchukiwa bila sababu huta ziona tena.
Natumai hivi sasa upo tayari kuokoka ili Yesu awe Msaada wako sasa. Kama ndio Fwatisha maneno haya kwa Imani, Sema BWANA YESU, NINAKIRI, YAKWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA WEWE NI MUNGU NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, INGIA SASA NDANI YANGU NA UNIOKOWE. AMENI.

Hongera kwa kuokoka natafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
MAWASILIANO: SIMU +255 759 859 287. WEB: www.mwanakondooinjili.blogspot.com

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni