Jumanne, 30 Mei 2017

YESU ANAKUJA.

 Na Mtumishi Oscar Samba.
(MWANAKONDOO Ministry)
Ni kweli ndugu yangu Ujio wa Yesu Kristo huu karibu mno na anakuja ili kuuhukumu ulimwengu hali itakayotoa maamuzi ama hatima ya maisha yako. Kama utaenda mbinguni ama Jehanamu ya Moto.

Kumbuka waendao mbinguni ni wale waliomwamini kama Bwana na mwokozi wa Maisha yao. Na kama hauja fanya hivyo ni wangu wito kumua hivyo sasa kwani ukifa hutakuwa na uamuzi katika hilo tena.
Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.

11 Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.
Kwa hiyo ndugu yangu, ni yangu rai kukutaka sasa kumuamini huyu Yesu Kristo ili uipate hiyo nafasi ya hukumu ya haki na kumbuka akija akikukuta ungali ulimwenguni atakunyakua na moja kwa moja utakuwa naye mbinguni.
Natumai hivi sasa upo tayari kuokoka ili Yesu awe Msaada wako sasa.

Kama ndio Fwatisha maneno haya kwa Imani, Sema BWANA YESU, NINAKIRI, YAKWAMBA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NA WEWE NI MUNGU NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, INGIA SASA NDANI YANGU NA UNIOKOWE. AMENI.
Hongera kwa kuokoka natafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.

MAWASILIANO: SIMU +255 759 859 287. WEB: www.mwanakondooinjili.blogspot.com

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni