Jumanne, 12 Desemba 2017
Jumanne, 30 Mei 2017
YESU ANAKUJA.
Na Mtumishi Oscar Samba.
(MWANAKONDOO Ministry)
|
Kumbuka
waendao mbinguni ni wale waliomwamini kama Bwana na mwokozi wa Maisha yao. Na
kama hauja fanya hivyo ni wangu wito kumua hivyo sasa kwani ukifa hutakuwa na
uamuzi katika hilo tena.
Warumi 10:9
Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni
mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.
10 Kwa maana
kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Jumatatu, 29 Mei 2017
UHAKIKA BAADA YA KUFA.
Na Mtumishi Oscar Samba. |
(MWANAKONDOO Ministry)
Ni jambo
jema kuwa na uhakika wa maisha utakayo ishi ama sehemu utakayoenda mara baada
ya kufa. Na uhakika huo unatokana na wewe jinsi ulivyo amua kuyaishi maisha
unayoishi hivi sasa.
Maandiko yanasema
wazi ya kwamba mara baada ya kufa ni hukumu, ikiwa na maana huwezi kutubu baada
ya kufa ama hakuna atakayekuamulia mahali pakwenda mara baada ya kifo chako
nikiwa na maana ya kwama hata ndugu zako wangekupenda na kukuombea kwa jinsi
gani bado isingalikupa tiketi ya kubadilishiwa maisha ama sehemu upaswapo
kwenda.
NINA MANTIKI
YA KWAMBA, UWAMUZI WA UTAENDA WAPI UNAFANYIKA UNGALI HAPA DUNIANI NA SIO BAADA
YA KUTOWEKA AMA KUNYAKULIWA. USIKUBALI KUDANGANYWA NA WIMBI LA UONGO WA MCHANA
YA KWAMBA ETI UTAOKOKA MARA BAADA YA KUFA, AU UTATUBU UKIFA. HUO NI UWONGO WALA
BIBILIA HAIJASADIFU JAMBO HILO.
Ni yangu rai
kukutaka leo kuwamua mahali utakapo kwenda, Na kumbuka kuwa njia zipo mbili. 1.
Kwanza ni ile ikupelekayo mbinguni na njia hiyo ni kumuamini Yesu. 2 Ni
MKIMBILIE YESU.
Na Mtumishi Oscar Samba |
(MWANAKONDOO
Ministry)
Haijalishi
unakumbana na jambo gani, ama unaishi maisha ya aina gani,? Jamii uliyonayo
inakuheshimu ama kukudharau. Ila ujumbe ambao Mungu amenipa siku ya leo ni huu;
MKIMBILIYE YEYE.
Ukifika kwa
Yesu kila kinachokusumbua kitakoma, magonjwa, mateso ya kimaisha, ugumu wa
kiuchumi, ndoa kusumbua, taabu za kukataliwa na kutengwa na ndugu. Ama ni tabia
za ukahaba, umalaya, wizi ulevi na hata ile ambayo hakuna nayeijua na nivigumu
kumwambia mtu mwingine yeyote na mimi siwezi kuitaja hapa maana kimaadili sio
vyema.
Katika hayo
yote wewe mwendee YESU naye atakusaidia maana amesaidia wengi ikiwemo yule mwanamke
aliyeonekana najisi kwa kunuka damu za mwezi na zilimtoka kwa muda wa miaka 12.
Jumamosi, 27 Mei 2017
YESU ANAKUPENDA
Na Mtumishi Oscar Samba. |
Hajui kumchukiwa
mtu, hata kama ni Kahaba, Mlevi, Mwizi, Mtukanaji, jamii inamuona kama Kichaa
ama aliyechanganyikiwa na Maisha ama kurukwa na Akili.
Ijumaa, 26 Mei 2017
NJOO KWA YESU.
Na Mtumishi Oscar Samba
|
Huyu Yesu
ninayemtaja mbele yako amewawezesha wengi kutoka katika adha kama hizo, wapo
waliokuwa wezi akawaokoa, akiwemo yule mwizi pale msalabani, makahaba, akiwemo
Rahabau. (Waebrania11:31 Kwa imani Rahabu,
yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale
wapelelezi kwa amani )
Na wewe mkaribishe
Yesu Kristo leo moyoni mwako kwa amani ili akuokowe na kisha kukutoa katika
hayo maangamivu ya kudharauliwa au kutengwa pia kuwa hatarini kupata magonjwa
kama UKIMWI na madhara kama yakifo ama kubaguliwa daima.
Yesu huyu
aliyemtoa Paulo Mtume aliyeitwa Sauli kwenye tabia ya uwaji anaweza kukusaidi
na wewe. Natumai hivi sasa upo tayari kuokoka ili Yesu awe Msaada wako sasa.
Kama ndio
Fwatisha maneno haya kwa Imani’ Sema BWANA YESU, NINAKIRI, YAKWAMBA MIMI NI
MWENYE DHAMBI, NA WEWE NI MUNGU NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, INGIA SASA NDANI
YANGU NA UNIOKOWE. AMENI.
Hongera kwa
kuokoka natafuta kanisa la watu waliokoka ukasali hapo.
MAWASILIANO:
SIMU +255 759 859 287. WEB: www.mwanakondooinjili.blogspot.com
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)