Jumatatu, 20 Oktoba 2014

MAMBO MAKUU NNE (4) KATIKA UOKOVU WAKO


Wapili kutoka kushoto ndie Mtumishi Jeremiah Mlawa akiwa na watumishi wenzake katika maeneo ya Ibada, (Picha na Makitaba)
Na Mtumishi Jeremiah Mlawa
1.Uwe na Imani,Hakikisha ndani ya uokovu wako uwe ni mtu wa  imani,jiamini na pia amini sehemu unayoabudu.
2.Uwe Mkweli,Epuka kuwa muongo na penda kuwa mkweli kwa kushuhudia kweli ya MUNGU,pia usiwe mzungumzaji kwa mtu ambaye unajua atahadhiri uokovu wako.Unapo mshuhudia mtu kuhusu uokovu hakikisha wewe mwenye ni msafi ndani ya moyo wako na ukifanya hivyo jina la MUNGU halitatukanwa na ushuhuda wako utakuwa barua.
3.Uwe Mtii,Hakikisha kwenye eneo unalolelewa unatii unaloambiwa,usiwe mwepesi wa kuitikia na kutokutii.Unapo weka ahadi kwa mtumishi ama mpendwa hakikisha unatii.Penda kutii muda wako katika maswala yako yakimaisha kama ibada inaanza saa 2 kamili hakikisha unatekeleza ama kutimiza hilo,Baraka za MUNGU huenda na wampendao.
4.Uwe ni Mtu wa Haki.Hakikisha kwenye maisha yako unaishi kwa haki na watu wote,na mwenendo wako uwe wa haki,tafuta amani na watu wote.Usijiesabie haki kwa kumuona mtu Fulani ambae ni mwenye dhambi anahatia na wewe ni bora kuliko yeye,Mungu wetu ni Mungu wa wote wenye mwili.Kama unawaona wako kinyume wewe waombe.

Ukiyazingatia haya hakika hali yako ya kiroho itakuwa ya utofauti kwa viwango vikubwa mno.MUNGU wetu wa mbinguni na BWANA YESU akuwezeshe kutii hayo.

Jumanne, 7 Oktoba 2014

Biblia inasemaje juu ya kutoa fungu la kumi ama Sadaka ya Michango ?

Hawa ni wataalamu wa injili kwa watu wote GFAP wakiwa katika picha ya pamoja huko ROMBO KILIMANJARO

Jibu: Kutoa fungu la kumi ni jambo ambalo wakristo wengi hung’ang’ana nalo. Katika makanisa mengine kutoa fungu la kumi imesisitizwa kupita kiasi. Wakristo wengi pia hukataa kutii agizo la kutoa sadaka kwa Bwana. Kutoa fungu la kumi au sadaka inahitajika kuwa ni kitendo cha furaha na baraka. Lakini sivyo katika makanisa ya sasa.

Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale. Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).
(1 Wakorintho 16 : 1-24
16.1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi
fanyeni vivyo.
16.2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili
kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;)

Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho ni kitengwe kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa.

Ni watoe sawa na uwezo wao “ kulengana na pato lake.” Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi,

 Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). “ kila mtu niatoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung’uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda kwenye kutoa kwa moyo mkunjufu” (wakorintho wa pili 9:7).

Pia hilo andiko nalipeleka kwa wale watumishi wa MUNGU wanao wapangia watu kiasi cha kutoa hususani kwenye michango,hakika jambo hili sio jema kwani kutoa kwa Toka KWA BWANA na haipendezi kumpangia mtu atoe nini bali kama alivyo sikia MOYONI mwake.

Pia katika makanisa ya leo usipo toa wanakuona kama mtu asiye endana nao yaani ajenti au msaliti hili sio sahihi kwani mtu kama mimisiwezi kutoa bila kusikia kwa hiyo hata msisitizo wakibina damu huwe mkubwa kiasi gani ni lazima nisikie kwa BWANA ama sivyo utakuwa tuu ni mchango na haifai kutoa kisha kunung'unika.

Siku njema na endelea kuetmbelea www.mwanakondooinjili.blogspot.com

USUHUDIAJI WA MTU KWA MTU KANISA LA TAG VCC ARUSHA

NA mama Mcungaji CATHERINE MBUGHI
Kushoto ndie mama Mchungaji Catherini Mbughi akisisistiza jambo la MUNGU katika jukwaa la Injili na kulia ndie Baba Mchungaji Aloice Mbughi.Picha na Makitaba.

Ninayo furaha ya hali ya juu kukukaribisha ewe msomaji wa blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com katika ujumbe huu wa leo kama ulivyotolewa kwenye kanisa la VCC na huyo mtumishi wa MUNGU kwenye mafundisho ya asubuhi ya wanafunzi na maandiko.

Ninae kuandikia ujumbe huu na kukuletea ni mimi OSCAR SAMBA na moja kwa moja tuzame kwenye somo letu la leo ambalo linalenga kukutia moyo wewe uliye okoka kuhusu kuwashuhudia wengine.

Luk 10:23-26
10.23 Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.
10.24 Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona
ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.
10.25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi
uzima wa milele?
10.26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?

Mpendwa kumbuka kuwa Inatupasa kuwashuhudia watu wote, Yohana 3:16, 3.16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.                    

,Unapo mshuhudia mtu msome NENO la Mungu kwani ndio silaa yetu na haikupasi kwenda vitani bila silaa.
Yohana 14.15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.Mpendwa andiko hili yatupasa kuhakikisha ya kwamba tunalishi hili kama kweli tunalipendana, kwa kuanza kushuhudia, na hii sio amri tuu bali pia ni agizo kuu.

Waambie ya kwamba mshahara wa dhambi ni mauti wala usiwafiche waeleze kuhusu jehanamu na pia wakumbushe uzuri wa mbinguni na waambie mbingu ipo kwa ajili yao tuu kama wakiamini.

Ukisha maliza muulize je, upo tayari kumapa YESU maisha yako akisema ndio muongoze sala  ya toba na akisema laa mulize na sema nae kuhusu hatima ya maisha yake nakumuliza je, anafahamu nini kuhusu hatima ya maisha yake baada ya kufa,mkumbushe kwa herufi KUBWA na msisitizo kinywani kuwa ni hukumu na hukumu yake MUNGU ni ya HAKI.

Mpe mfano wa tajiri na Lazaro kwani mara baada ya kifo kila mmoja alivuna alichopanda, Lazaro mbinguni tena kifuani mwa Ibrahimu na Tajiri motoni.

Hakika kupitia NENO la Mungu inawezekana kuwafanya watu kuingia mbinguni.Maandiko tuliyoyasoma hapo juu yanatutaka tuwapende jirani zetu kama Nafsi zetu pia “1 YOHANA 4-20-21   4.20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana
asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
4.21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Kwa hiyo yatupasa kutimiza andiko hili kwa Moyo wote kwani upendo wa kweli kwa Mungu wetu huanza kwa kumpenda jirani yako na upendo wa kweli kwa jirani yako uliyo na matendo ni kumwambia habari za YESU.

Weka mpango na mikakati yakuhakikisha yakwamba ndugu zako na rafiki zako wanaokoka,usikubali waende huko kwani kunatisha mnoo.
Mliliye YESU nasema nae kuhusu ndugu na jamaa zako lakini pia toka ka’a waambie hao watu ya kwamba YESU anaokoa.

MAMBO MUHIMU
1.Uwe na huruma ya KIMUNGU ndani yako,hakikisha unaguswa na tabu zao na mateso yao
2.Uwe na upendo wa MUNGU ndani yako YOHANA 3:16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Usikubali juma hili lipite bila kuwaambia habari za YESU,ukikutana nae njiani ama popote pale mwambie YESU anampenda.Hata kama hataokoka leo lakini hakikisha unampandia NENO.
Upendo unagarimu,upendo unahitaji kujitoa kwa hiyo hakikisha unaingi gharama kwa kusugua goti ili watu waende mbinguni.Litumie NENO kwani hili NENO linauwezo wa kumuokoa na kumbadilisha kumbuka IMANI huja kwa kusikia kwa mantiki hiyo hilo NENO huweza kufanyika uponyaji kwake.
Kuna vilio vya aina mbili cha kwanza—ni cha mtu aliyeomba maji akiwa Jehanamu na B yake ni cha mtu aliyeomba ndugu zake wasiende jehanamu.
Luka 16:19-31
“16.19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula
sikuzote kwa anasa.
16.20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi,
16.21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata
mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake.
16.22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye
akafa, akazikwa.
16.23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali,
na Lazaro kifuani mwake.
16.24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake
majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.
16.25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika
maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.
16.26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku
kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.
16.27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,
16.28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.
16.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.
16.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.
16.31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.”

Embu jiulize angalikuwa ni ndugu yako yuko huko jehanamu ungali jisikiaje ?
Na kilio chapi ni cha mtu uliyemshuhudia na kukataa kuokoka..
Zingatio kuu la somo la leo : TUKIKOSA HURUMA HATUTA VUNA
Naam hadi kufikia hapo ndio mwisho wa ujumbe huu tafadhali endelea kutembelea blogu hii ya www.mwakasegeinjili.blogspot.com kwa makala na habari zaidi.Pia kumbuka siku chache zijazo blogu hii itakuwa na na jina jingine ambalo ni www.ukombozig.blogspot.com na kwa sababu zaidi soma habari iliyopita.