Jumatatu, 12 Mei 2014

Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe;JEHANUM YA MOTO


Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org
Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO LA 6: JEHANUM YA MOTO
Yesu Kristo anatufundisha waziwazi kuhusu Jehanum ya moto, akituonya kumwogopa Mungu mwenye uwezo wa kututupa Jehanum. Anaendelea kutuonya kwamba, ni heri kukubali lolote lile litupate kuliko kwenda kwenye mateso makali ya Jehanum (LUKA 12:5, MATHAYO 5:22, 29-30). Maandiko pia yanaendelea kusisitiza kwa msisitizo mkubwa kwamba, ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai na kutupwa katika Jehanum ya moto (WAEBRANIA 10:26-27, 31). Jehanum hii ya moto inaitwa pia kuzimu (ZABURI 9:17) na tena inaitwa Tofeni (ISAYA 30:33). Hatupaswi kulipuuza jambo hili na kulifanya juu juu tu. Kwa sababu hii, leo, tutajifunza kwa undani kuhusu Jehanum ya moto, na tutaligawa somo letu katika vipengele vinne:-

(1) HUKUMU BAADA TU YA KUFA

(2) JEHANUM YA MOTO IKO WAP?

(3) HALI HALISI YA JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO

(4) JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO

( 1 ). HUKUMU BAADA YA KUFA

Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu (WAEBRANIA 9:27). Watu wanaofundisha kinyume na kweli ya neno, hufundisha kwamba mtu anapokufa analala tu na hakuna lolote la hukumu ya mara moja. Wanatumia maandiko yanayozungumzia kulala kwa kuyatafsiri isivyo (MATHAYO 27:52; 1 WAKORINTHO 15:20; YOHANA 11:11-14 n.k ) na pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo ni kwamba kinachobaki kaburini ni mwili tu. Nafsi na roho ya mtu huondoka kwa kuvalishwa mwili mwingine ( 1WAKORINTHO 15:40 ). Mwili unaobaki kaburini ndiyo ambao umelala haujui lolote na hauna kumbukumbu, lakini pasipo mwili huo mtu atamwona Mungu ikiwa ameishi katika mapenzi yake(AYUBU 19:26). Mwili hubaki kaburini, lakini roho ya mtu huondoka (MHUBIRI 12:7). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu mara tu ya kufa huchukuliwa mbinguni na malaika kwa kutumia magari maalum ya mbinguni (LUKA 23:43; 16:22; 2WAFALME 2:11-12; ZABURI 68:17; WAEBRANIA 1:7, 14). Ikiwa ameishi katika dhambi hukumu yake huwa kutupwa katika Jehanum ya moto mara tu baada ya kufa (MITHALI 9:13-18; ISAYA 5:11-15; MITHALI 17:24-27).

( 2 ). JEHANUM YA MMOTO IKO WAPI?

Mtu anapokufa tu, huwa kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni, hata hivo ikiwa jina lake haliko katika kitabu cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni na hulazimika kukamatwa na kutupwa Jehanum (UFUNUO 19:20; 20:10). Mbinguni ni juu (mbingu ya tatu) lakini kuzimu au Jehanum ya moto ni chini (pande za chini za nchi) 2WAKORINTHO 12:1-4; ITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14.

( 3 ). HALI HALISI YA JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO

Jehanum ya moto ni kuzimu au shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Moto huu huwashwa mfululizo kwa pumzi ya Bwana (ISAYA 14:15; 30:33). Moto ni mkali kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani, uwe gesi, umeme, makaa yam awe au lolote jingine (WAEBRANIA 10:27). Moto huu ni mweusi unaosababisha giza na kufanya mtu awaone wenzake wachache tu wa karibu naye (MATHAYO 11-12; 22:13; 25:30 YUDA 1:6). Moto huu una uwezo wa kula na kutafuna, kwa hiyo huwatafuna au kuwala wale walioko motoni (KUMBUKUMBU LA TORATI 32:22; WAEBRANIA 10:36-27). Hata hivyo, kama jinsi ambavyo chumvi inavyozuia nyama kuharibika, moto humtafuna mtu lakini hamaliziki (MARKO 9:43-49). Ni moto wa milele (MATAYO 25:41). Mafundisho potofu ysnswafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa au kupotea na kuangamia kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 ( kuangamizwa ) na YOHANA 3:16 ( kupotea ). Kuangamia hakumaanishi kualizika kabisa (ESTA 4:16). Kondoo akipotea haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na mchungaji (angalia ISAYA 57:1-3). Vilevile neno “kuharibu” linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni la kuzdhibu vikali ( 1WAKORINTHO 3:16-17 ). Waalimu hawa wa uongo hufundisha pia kwamba ati watu watatoweshwa kama moshi baada kwa kuunguzwa kwa kutumia ZABURI 37:20. Kutoweshwa hapa ni kutenganishwa mbali na Mungu. Moto wa milele, huambatana na madini yanayoitwa kiberiti (lugha ya kitaalam, “sulphur”). Madini haya yakiwaka huwa kama mpira na hutoa harufu kama ya mayai yaliyooza. Harufu ya namna hii inafunika kuzimu yote. Siyo hayo tu, katika moto huu wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi katika miili yao wakiingia na kutoka. Hii hufanya sura zao kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA 14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24). Jehanum ya moto, huitwa pia mauti ya pili(UFUNUO 21:8). Uchungu wa mauti unaompata mtu anapokufa, huwa juu ya mtu motoni, milele na milele (UFUNUO 20:10). Watu walioko motoni hujawa wakati wote na vilio na tena husaga meno yao kama mtu anayeona baridi kali MATHAYO 8:12). Kuzimu, urikalo ni pigo lif urikalo ambalo huwachukua wenye dhambi asubuhi, mchana na usiku (ISAYA 28:15, 18-19). Walioko motoni wanajifahamu, na kuwakumbuka wenzao waliowaacha duniani na tena hutoa ndimi zao nje wakitamani maji kidogo kupoza ulimi (LUKA 16:19-24). Juu ya yote hayo, katika vilio vyao, humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Yeye amekwishasema, “Nami jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma”(EZEKIELI9:10;8:18).

USEMI NA FIKRA ZA WALE WALIOKO MOTONI

Watu walioko motoni hutamani mtu mmoja kati yao aje awashuhudie ndugu zao ili wayoache dhambi na kukwepa mateso yao (LUKA 16:27-31). Wale walioko huko wajiopata mafundisho haya kabla, husema, “Jinsi nilivyochukia maonyo, na na moyo wangu ukadharau kukemewa; wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, wala sikuwategea sikio langu walionifundisha (MITHALI 5:11-13)” Wakimwona yeyote anayejiunga nao, humwambia, “Jew ewe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe ummekuwa kama sisi!” ( ISAYA 14:9-10).

WALIO MBINGUNI HUPEWA NAFASI YA KUWACHUNGULIA

Walioko mbinguni watatoka kidogo kuwaangalia (ISAYA 66:24) ila hawatakuwa na machozi yoyote juu yao.

TOFAUTI KATI YA JEHANUM YA MOTO NA ZIWA LA MOTO

Jehanum ya moto ni tofauti na ziwa la moto linalotajwa katika UFUNUO 20:14-15; 21:8 kwa jinsi ileile mbingu ya sasa ilivyo tofauti na mbingu mpya inayotajwa katika UFUNUO 21:1. Ziwa la moto kwa sasa halina mkazi ndani yake. Watakaokuwa wa kwanza kuingia humo watakuwa mnyama (Mpinga Kristo)na nabii wa uongo (UFUNUO 19:20). Kisha atafuata ibilisi ambaye atatupwa humo baada ya vita ya Gogu na Magogu (UFUNUO 20:7-10). Baada ya hapo kutafuata hukumu ya jiti cha enzi, kikubwa cheupe. Hukumu hii itatolewa baada ya ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu ambao utawafufua walioko Jehanum ya moto.Baada ya hawa kuelezwa kwa nini wamehukumiwa adhabu ya matesoya milele, ndipo watakapotupwa katika ziwa la moto. Mateso yaliyoko ziwa la moto ni zaidi sana kuliko mateso ya Jehanum ya moto. Ni kama Jehanum walikuwa mahabusu na sasa wanapelekwa gerezani. Kama mbingu mpya itakavyokuwa nzuri zaidi kuliko mbingu ya sasa, vivyo ziwa la moto litakuwa na mateso yaliyokithiri kuliko Jehanum ya moto.

( 4 ). JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO

1 .Kuungama dhambi na kuziacha (MITHALI 28:13).

2. Kulishika Neno la Mungu kwa kufanya maagizo yote ya Mungu na kuwakata wafariji wenye kutaabisha wanaosema kufanya hili na lile siyo lazima ( YOHANA 8:51; ZABURI 119:6; AYUBU 16:1-2 ).

3. Kutohesabu sheria kuwa kutu kigeni. Kukubali kuongozwa na sheria ya Kristo. Hakuna mwanafunzi asiyeishi kwa sheria ( HOSEA 8:12; WAGALATIA 6:2; ISAYA 8:16 ).

4. Kuwa mtakatifu na kutoifuatisha namna ya dunia hii katika mavazi, usemi, matendo n.k. ( WAEBRANIA 12:14; WARUMI 12:2; YAKOBO 4:4; 1YOHANA 2:15-17 )

JE! WEWE NAWE UMEKUWA DHAIFU KAMA SISI!

ISAYA 14:9-10
Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/01/02/kunyakuliwa-kwa-kanisa/
2. DHIKI KUBWA
https://davidcarol719.wordpress.com/dhiki-kubwa/
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/taji-kwa-watakatifu-na-harusi- ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
https://davidcarol719.wordpress.com/2013/02/10/kuja-kwa-yesu-kristo-mara-ya-pili-duniani-na-vita-ya-har-magedoni/
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
https://davidcarol719.wordpress.com/miaka-1000-ya-utawala-wa-yesu-kristo-duniani-na-vita-vya-gogu-na-magogu/
6. UFUFU WA WAFU
https://davidcarol719.wordpress.com/187-2/
7. JEHANUM YA MOTO
https://davidcarol719.wordpress.com/jehanum-ya-moto/
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/229-2/
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
https://davidcarol719.wordpress.com/mbingu-mpya-na-nchi-mpya/

. . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Zipo Baraka nyingi kwa yeyote atakaye “share “ ujumbe huu katika Facebook,Twitter n.k, kwa ndugu, jamaaa na marifiki ili nao wapate nafasi ya kusoma ujumbe huu na kubarikiwa kama wewe ulivyo barikiwa. Kwasababu hii share ujumbe huu kwa kubonyeza neno“ share” lililopo chini ya “note” hii, kwa kufanya hivyo ujumbe huu utafika kwa watu wengi. Hakika, Baraka za Mungu zitakuwa nawe.

UBARIKIWE NA BWANA YESU!!!

ISRAEL HOUGHTON KUIMBA NCHINI UGANDA MWEZI UJAO, HAKUNA KIINGILIO


Watoto Children Choir namba 66 wakiimba kanisani kwao kabla ya kuelekea nchini Australia kwa ziara wiki mbili zilizopita.
Nyota wa muziki wa injili duniani Israel Houghton kutoka nchini Marekani anatarajiwa kuwa mwimbaji mwalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 30 ya huduma ya kanisa la Watoto Uganda pamoja na miaka 20 ya huduma ya wanawake na watoto kupitia Watoto child care ministries zote zikiwa chini ya kanisa la Watoto ambalo umaarufu wake umetokana na kwaya ya Watoto children chini ya waanzilishi wa huduma hiyo Gary na Marilyn Skinner zitakazofanyika mwezi wa sita nchini

humo.

Israel na kundi lake la New breed wanatarajiwa kuimba siku ya alhamis tarehe 5 katika kanisa la Watoto west tukio ambalo halitakuwa na kiingilio lililopewa jina la 'Watoto Big Party'. Hii itakuwa si mara ya kwanza kwa mwimbaji huyo kuimba jukwaa moja na Watoto children choir ambao amekuwa akikutana nao sehemu mbalimbali. Mwimbaji huyo atakuwa nchini Uganda wiki moja baada ya kumaliza tamasha lake kubwa la uimbaji litakalofanyika jijini London nchini Uingereza tarehe 27 mwezi wa tano akiwa na kundi lake kamili.

Haya kwa wale wapenzi wa mwanamuziki huyo, ni kujipanga nauli ya kwenda na kurudi na sehemu ya kufikia bila kusahau chakula, onyesho halitakuwa na kiingilio.

Jumamosi, 10 Mei 2014

KAKOBE; UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU



Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO: UTHIBITISHO KUWA YESU NI MUNGU

Ni muhimu kufahamu kuwa Yesu Kristo ni Mungu.Ikiwa sisi ni wanafunzi wa Biblia tusiwe kama wengine wanaosema kuwa Yesu si Mungu.Kama huna moyo wa jiwe kama wengine waliotiwa upofu kiroho na kushindwa kuyaelewa maandiko,Je,unaamini kuwa Yesu ni Mungu? Yesu ni Mungu na ushahidi mwingi wa maandiko upo.

Somo hili lipo katika vipengere vinne vifuatavyo:-
KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA BIBLIA.
SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA NI MUNGU.
YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI MUNGU PAMOJA NASI.
YESU MWANA WA MUNGU.

Kipengere cha kwanza,

1.KUTAJWA KWA YESU KRISTO NI MUNGU KATIKA MAANDIKO.Hapa tunaona maandiko yakimtaja Yesu KriNasto waziwazi kuwa ni Mungu. Katika ( 1YOHANA. 5:20 ) “Nasi twajua kuwa Mwana wa Mungu amekwisha kuja,naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli,nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli.,yaani ndani ya Mwana wake Yesu Kristo.Huyu ndiyeMUNGU WA KWELI NAUZIMA WA MILELE”.. Pia katika ( YOHANA 20:26-29 ) “basi,baada ya siku nane,wanafunzi wake walikuwamo ndani tena,na Tomaso pamoja nao.Akaja Yesu na milango ilikuwa imefungwa,akasimama katikati,akasema,Amani iwe kwenu.Kisha akamwambia Tomasolete hapa kidole chako;uitazame mikono yangu;ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu;wala usiwe asiyeamini;bali aaminiye.Tomaso akajibu akamwambia,BWANA WANGU NA MUNGUWANGU..Yesu akamwambia,wewe kwa kuwa umeniona umesadiki;wa heri wale wasioona wakasadiki”.YESU KRISTO MUNGU MKUU, ( 1TITO 2:13 ) “Tukilitazamia tumaini lenye mafunuo yaKRISTO YESU MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU”.. YESU NI MUNGU aliyejifunua katika mwili (WARUMI 9:5 ) “Na katika hao alitoka KRISTO KWA NJIA YA MWILI,NDIYE ALIYE JUU YA MAMBO YOTE,MUNGU,MWENYE KUHIMIDIWA MILELE.AMINA..Mhalifu msalabani alimwita YESU Mungu na kumuomba YESU atakapokuwa katika ufalme wake amkumbuke mharifu huyo”. ( LUKA 23:39-43 ).Yesu hakukataa kuwa SI MUNGU bali alisema,Amini nakuambia leo hivi,utakuwa pamoja nami peponi.YESU NI MUNGU ALIYEKUJA DUNIANI .( WAFILIPI 2:5-6 ) “Ambaye yeye mwanzo alikuwan yuna namna ya Mungu,naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho,bali alijifanya kuwa hana utukufu,akatwaa namna ya mtumwa,akawa ana mfano wa wanadamu”.YESU alijita-mbulisha kwao kuwa ni MUNGU lakini hawakuelewa ( YOHANA 10:30-33 ) “Yesu akawajibu,kazi njema nyingi niwewaonyesha zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu,kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe;bali kwa kukufuru,na kwasababu wewe uliye.mwanadamu wajifanya kuwa Mungu. Wayahudi walisema anakufuru kwa kusema kuwa yeye ni Mungu.Kimsingi Yesu ndiye Baba mwenyewe ndio maana anasema huwezi kumtenganisha na Baba; ukimwona yeye umemuona Baba. ( YOHANA 14:7-9 )


Katika mstari 8 na 9 Filipo akamwambia,Bwana,utuonyeshe Baba yatutosha. Yesu akamwambia,Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote,wewe usinijue,Filipo?

Ikiwa tu wanafunzi wa Yesu hatupaswi kubabaishwa na watu ambao hawana Roho wa Mungu.Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kusema Yesu ni Mungu..Kwasababu hiyo,wanatumia akili tu.Hawa ni watu wa tabia ya asili ambao hawawezi kuyaelewa mambo ya kiroho ( 1WAKORITHO 2:14 ) “Basi,mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kuyapokea mambo ya Roho wa Mungu;maana kwake ni upuuzi;wala hawezi kuyafahamu;kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni”

2.SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU.

1.YESU NI MUUMBAJI.

Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake ( YOHANA 1:3,14 ) “vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili;nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli”.Yesu aitwa Neno la Mungu (UFUNUO 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(YOHANA 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (WAKOLOSAI 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani.Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.

2.YESU ALIKUWEPO KABLA YA VITU VYOTE KUWEPO DUNIANI.

( WAKOLOSAI 1:17 ) “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote;na vitu vyote hushikamana katika yeye”.(MIKA 5:2 ) “Basi,wewe Bethlehemu,Efrata,uliyemdogo kuwa miongoni mwa maelfu za Yuda;kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale;tangu milele“.

Yesu Kristo alikuwako kabla ya Nabii Ibrahimu kuwako(YOHANA 8:52-58). Watu walioambiwa maneno hayo n a Yesu mwenyewe wliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwa anakufuru.Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho,( YOHANA 4:24)..YOHANA 17:5,24.WAEBRANIA 7:3 ).Imasema “hana baba,hana nana,hana wazazi,hana mwanzo wa siku zake,wala mwisho wa uhai wake,bali amefananishwa na Mwana wa Mungu;huyo adumu kuhani milele”.YESU ni alfa na omega,wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (UFUNUO 22:13).Bali kwa damu ya thamani,kama ya mwana-kondoo asiye na ila,asiye na waa,yaani ya Kristo.Naye amejulikana kweli tangu zamani,kabla haijawekwa misingi ya dunia,lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yetu ( 1PETRO 1:19-20 ).


3.YESU NI MTAWALA JUU YA YOTE. HII NI SIFA YA MUNGU PEKEE.

(YOHANA 330 ) “Yeye ajaye kutoka juu,huyo yu juu ya vyote.Yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia,naye anena mambo ya duniani,yeye ajaye kutoka mbinguni yuu juu ya yote” . ( YOHANA 13:13 ) “Ninyi mwaniita ,Mwalimu, na Bwana;nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo“. ( WARUMI 14:9 ) “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii,awamiliki waliokufa na walio hai pia”. Nenokumiliki ni kutawala sifa ya kutawala ni sifa ya Mungu pekee.




4,YESU KRISTO NI ZAIDI YA MTU YEYOTE AU NABI AU MTUME YEYOTE YULE..

( WAEBRANIA 3:1-7 ) “Mustari 3 unasema,Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahiliutukufu zaidi kuliko Musa,kama vile yeye atengenezayenyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”..Anayezungumziwa hapa ni Yesu Kristo Mungu muumbaji. YESU ,ameketi mkono wa kuume wa ukuu huko mbinguni (WAEBRANIA 1;3-4).

5,YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WALIMWENGU (WATU) WOTE.

( ZABURI 58:11 ), ‘Hakika yuko Mungu anayetawala katika dunia“. (UFUNUO 18;8 ) “Kwasababu hiyo,mapigo yake yatakuja katika siku moja,mauti na huzuni na njaanaye atateketeza kabisa kwa moto.Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“.Tene ndiye atakaye ihukumu Dunia yote “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote,bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.(MATHAYO 25:31-32 ) “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake,namalaika watakatifu wote pamoja naye,ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake,naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi” .(MATENDO 10:42 ) “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( WARUMI 2:16 ) “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na injili yangu,kwa Kristo Yesu“.( 2TIMOTHEO 4:1 ) “Nakuagiza mmbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu,atakayewahukumu waliohai na waliokufa;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.

6.YESU HABADILIKI TENE HANA KIGEUGEU. {WAEBRANIA 13:8} “Yesu Kristo ni yeye yule jana na leohata milele“. ( WAEBRANIA 1:10-12 ) “Wewe ,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi.Na mbingu ni kazi ya mikono yako;Hizo zitaharibika,lakini wewe unadumu;Nazo zote zinachakaa kama nguo,Na kama mavazi,utazizinga,nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,na miaka yako haitakoma“. ( MALAKI 3:6 ) “Kwa kuwa mimi,Bwana,sina kigeugeu” ( ZABURI 102:26-27 ) “Hizi zitaharibika,bali wewe utadumu;Naam,hizi zitachakaa kama nguo;na kama mavazi utazibadirisha,nazo zitabadilika.Lakini wewe U yeye yule;na miaka yako haitakoma“. ( YAKOBO 1:17 ) “Kwake hakuna kubadilika,wala kivulu cha kugeukageuka”.
YESU YUPO KILA MAHALI ,KOTEKOTE DUNIANI.

( MATHAYO 18:20 ) “Kwa kuwa walipo wawili watatu,wamekusanyika kwa jina langu,mimi nipo papo hapo katikati yao”. Mwenye uwezo wa kukaa mahali pote ni Mungu.
YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI(MUNGU PAMOJA NA WANADAMU).

( MATHAYO 1:23-25 ) “Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lakeEmanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”.Tabia ya Yesu inaonyesha kuwa kama mwanadamu,kuzaliwa kwake kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Hapa tunaona jinsi alivyo na uwezo wa tofauti na wanadamu akiwa anafahamu mambo yote kabla akiwa duniani..Yeye pia ajua yote yaliyomo ndani ya moyo wa mwanadamu (YOHANA 6:64,YOHANA 13:1,YOHANA 13:11,YOHANA 18:4,YOHANA 19:28).Tena Yesu alitabiri kabla jambo kutokea,pia alijitabiria mwenyewe yatakayomtokea mbele (MARKO 8:31,LUKA 9:22,LUKA 12:50,LUKA 22:37,LIKA 24:7-26,YOHANA 3:14,YOHANA 10:17-18,YOHANA 7:33,YOHANA 13:33,YOHANA 14:28,YOHANA 17:11,YOHANA 16:5,10,16,18 ).

Yesu aliabudiwa na kusujudiwa akiwa hapa duniani,Sifa ya kuabudiwa na kusujudiwa ni ya Mungu pekee hivyo Yesu ni Mungu.(MATHAYO 4:10).
Hata malaika wote wanamsujudia Yesu (UFUNUO 22:8-9,WAEBRANIA 1;6).
Ndiyo maana Yesu alisujudiwa akiwa mtoto mchanga alipozaliwa (MATHAYO 2:11,MATHAYO 14:33<LUKA 24;52).
Hata pepo wachafu walimsujudia Yesu (MARKO 5:2,6).

YESU ALIKUWA MWANADAMU ALIPOKUWA DUNIANI


A: Alizaliwa na bikira Mariamu(mwanadamu) ( LUKA 2:3-7 ).

B: Aliongezeka kimo ( LUKA 2:40-42-52)

C: Aliona njaa kama watu wengine ( LUKA 4:2)

D: Alilala usingizi kama binadamu wengine( LUKA 8:23)

E: Alikuwa na viungo kama binadamu( LUKA 24:36-40)

F: Alikula chakula ( LUKA 24:41-43)

G: Alichoka kama mwanadamu ( LUKA 4:6; WAEBRANIA 4:15 : 2:16-18
Msalabani alikufa kama mwanadamu hakufa kama Mungu ila alitupatanisha 1TIMOTHEO 2:5
Tunaona mama yake mariamu asema mimi ni mjakazi wa BWANA YESU ( LUKA 1:38-46-47)
Tunaona pia hapa wakati wamekusanyika kwa ajili ya maombi akiwemo na Mariamu waliomba kwa jina la BWANA wala si kwa jina la mariamu(MATENDO 1:13-15,1 YOHANA 4:1-2.

4:YESU MWANA WA MUNGU

Tunaona hapa biblia inatuambia YESU KRISTO ni mwana wa Mungu (YOHANA 20:30-31) hapa Yesu mwenyewe anasema yeye ni mwana wa Mungu ( MATHAYO 26:59-64; 16:13-17 ) , neno mwana linamzungumzia Yesu mwana siyo kuwa Mungu anazaa la hasha

Yesu anaitwa mwana wa Mungu kwa sababu alizaliwa kwa uweza wa R oho Mtakatifu. Hata sisi tumezaliwa kwa mara ya pili kwa roho tunapo mwamini Yesu Kristo hivyo tunahesabika kuwa ni wana wa Mungu.(WAFILIPI 2:14-15,YOHANA 1:12).Kwahiyo Yesu anapoitwa Mwana wa Mungu maana yake ni chapa ya Mungu (HUIOS) WAEBRANIA 1:1-3.Ndiyo maana hapa Yesu anawaambia wanafunzi wake,mumeniona mimi ;mumemuona Mungu,maana yake ndiyo hiyo (HUIOS) yaani chapa ya Mungu (YOHANA 14:7-9)
Tunaona hapa Yesu alisema Yeye ni Mwana wa Mungu (YOHANA 9:35-37)
Shetani naye anajua kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (MARKO 3:11,LUKA 4:41).
Malaika nao wanasema kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (LUKA 1:30-35)
Mungu mwenyewe anasema kuwa Yesu ni Mwanangu mpendwa (MATHAYO 3:17,MATHAYO 17:5 )

KUMKIRI YESU KRISTO KUWA NI BWAMNA

Matatizo yote yanayompinga Yesu Kristo kuwa si Mwana wa Mungu,inatokana mtu yeyote anakuwa hana roho wa Mungu (1yohana 4:15) na Mungu hayuko ndani ya mioyo yao (1YOHANA 2:23,LUKA 10:16)ndiyo maana maandiko matakatifu ya Mungu yanasema asiyemwamini Mwana hana uzima wz milele,hiyo adhabu ya milele inamkalia (YOHANA 5:23,YOHANA 3:36,YOHANA 5:11-13) Kwahiyo wanaomkataa Yesu Mwana wa Mungu hawawezi kushinda dhambi.Huwezi kushinda dhambi kama huamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu (1YOHANA 5:4-5,YOHANA 1:12).Ndiyo maana mtu mwenye dini tu hawezi kushinda dhambi kwasababu hajampokea Yesu Mwana wa Mungu (YOHANA 1:12) Wote wanaompokea wanapewa uwezo wa kushinda dhambi.Ni rahisi kuthibitisha ukweli wa maneno haya; wewe muangalie mtu yeyeyote wa dini tu bila Yesu,hana uwezo wa kushinda dhambi.Ni watukanaji,wazinzi,wenye tama n.k ingawa sala zao ni nyingi na ndefu lakini haziwezi kuwasaidia kushinda dhambi.Ni muhimu kufahamu kuwa ni Yesu peke yake aliyeishi duniani bila kutenda dhambi (WAEBRANIA 4:15).Hakuna wokovu katika mwingine (MATENDO 4:12).Hakuna uwezekano kwa mtu ambae hajamkiri Yesu Kristo kuingia mbinguni (YOHANA 14:6).Yesu ni njia na kweli n a nuzima………………………………………………………………………..

………………………………………………………………………………………………………..

Ni sifa ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14). Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi. Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi. Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”. Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

KAKOBE; YANIPASA NIFANYE NINI NIPATE KUOKOKA?

Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO LA MAKANISA YA NYUMBANI

SOMO LA 111 : YANIPASA NIFANYE NINI NIPATE KUOKOKA?

NENO LA MSINGI:

MATENDO YA MITUME 16:30, 32

“Kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, YANIPASA NIFANYE NINI NIPATE KUOKOKA? Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake”.

<><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><><

W


atu waliookoka katika Kanisa la Kwanza lililokuwa linaongozwa na Mitume, walijua sana jinsi ya kumweleza mtu maana ya wokovu hata yeye naye akaokolewa. Katika Neno hili la msingi, tunaona mtu mmoja akiuliza afanye nini apate kuokoka, na hapohapo anaambiwa neno la Bwana na kuelewa analopaswa kulifanya. Watu wote tuliookoka, ni wajibu wetu kuwaambia watu wote neno la Bwana linalohusu wokovu ili yamkini wote wapate kuokolewa. Jambo la huzuni ni kwamba watu wengi waliookoka, hawawezi kumweleza mtu mwingine neno la BWANA hata akaelewa, na yeye akaokolewa. Kanisa la Mungu halipaswi kuwa hivi na kuwaacha wengi wakiangamia! Basi, ni makusudi ya somo la leo la Kanisa la Nyumbani, kujifunza hatua kwa hatua yanayotupasa kufahamu katika kumwambia mtu neno la BWANA hata na yeye aokolewe. Ikiwa wewe uliyehudhuria leo katika Kanisa la Nyumbani hujaokolewa basi unapokuwa unajifunza somo hili hujaokolewa basi ni siku yako pia kuokolewa baada ya kufahamu yote yanayokupasa kufahamu na kuyafanya.

A: NINI MAANA YA NENO “KUOKOKA” AU “KUOKOLEWA?“

Kuokoka au kuokolewa, ni kunusurishwa, kuopolewa, kusalimishwa au kuponywa kutoka katika maafa makubwa yaliyo dhahiri kabisa kukupata. Inaweza ikawa kuponywa kutoka katika hatari ya kifo adhabu kali au madhara yoyote makubwa yaliyo dhahiri. Katika hali ya kukosa matumaini ya kukwepa maafa hayo yaliyo dhahiri, inapotokea ghafla njia ya kusalimika hapo inasemekana umeokoka.

ANGALIA MIFANO KATIKA BIBLIA:

Baada ya Yusufu kuuzwa na ndugu zake na kupelekwa kuwa mtumwa huko Misri,

ilitokea njaa kubwa sana katika ulimwengu wote wa wakati huo. Watu wengi mno walikufa kwa kukosa chakula, na kulikuwa hakuna matumaini. Ndugu zake Yusufu nao walikuwa katika hatari ya kifo. Kabla ya njaa, huko Misri Yusufu kwa uwezo wa ajabu wa Mungu, aliaminiwa na kuwa Waziri Mkuu wa nchi ya Misri na akatumiwa na Mungu kuhifadhi chakula kingi ambacho hatimaye, kilitumika kuwaokoa ndugu zake katika maafa ya kufa kwa njaa.

MWANZO 45: 5 – 7:

“Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinipeleka mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu. Maana miaka hii miwili njaa imekuwa katika nchi, na iko tena miaka mitano isiyo na kulima wala kuvuna. Mungu alinipeleka mbele yenu kuwahifadhia masazo katika nchi,NA KUWAOKOA NINYI KWA WOKOVU MKUU“.

Daudi akiwa katika hali ya hatari anaelezea juu ya hali ya mtu anayehitajika kuokolewa mtu ambaye yuko katika hatari ya kufa baada ya kuzama katika matope mengi na maji yakiwa yamefika nafsini mwake.

ZABURI 69:1 – 2:

“Ee Mungu, UNIOKOE, maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. Ninazama katika matope mengi, pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, mkondo wa maji unanigharikisha.”

Wakati wa Nuhu, Mungu akiwa amechukizwa na dhambi za watu wa wakati ule, aliwaonya watu juu ya maafa yatakayokuja, kuwaangamiza wote wasiomtii Mungu. Watu wote wakapuuza ujumbe huo, isipokuwa Nuhu aliyetii na kuunda Safina iliyotumika kumwokoa yeye na watu wa nyumba yake kutoka katika maafa ya kufa kwa gharika kuu. Watu wote walikufa kutokana na gharika hiyo isipokuwa Nuhu na wenzake saba waliookolewa katika maafa hayo.

WAEBRANIA 11:7:

“Kwa Imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu aliunda safina, APATE KUOKOA NYUMBA YAKE”.

B: MAISHA YA BAADAYE YA MTU MWENYE DHAMBI:

Mtu yeyote mwenye dhambi lazima atapata adhabu ya milele. Adhabu yake inaitwa MAUTI YA PILI auMAUTI YA MILELE ambayo ni kutupwa motoni na kuteswa milele. Hakuna mwenye dhambi atakayekwepa adhabu. Kila mmoja atapata mshahara huu wa dhambi, mauti ya milele au kutupwa Jehanum ya moto.

MITHALI 11:19 – 21:

“——- Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe—— Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu——-”.

EZEKIELI 18:4, 20:

“—-Roho itendayo dhambi itakufa————-”.

WARUMI 6:25:

“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.”

UFUNUO 21:8:

“Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao, ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo MAUTI YA PILI.”

Hakuna mtu yeyote mwenye dhambi yaani asiyekuwa na haki mbele za Mungu atakayeokoka katika maangamizo hayo. Kwa sasa mtu mwenye dhambi anaona kwamba yuko salama na kwamba amani iko kwake, lakini ghafla uharibifu wake utamwijia.

1 WATHESALONIKE 5:3:

“Wakati wasemapo, kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba wala hakika hawataokolewa.”

ZABURI 119:155:

“Wokovu u mbali na wasio haki kwa maana hawajifunzi amri zako (na kuzitenda)”.

C. NI NANI MWENYE DHAMBI?

Jibu ni kwamba kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke, kutokana na asili ya Adamu, yuko miongoni mwa wenye dhambi. Wote wamefanya dhambi. Kwa mtu mmoja Adamu, dhambi iliingia ulimwenguni; na WATU WOTE wakahesabiwa kuwa wenye dhambi. Kutokana na kila mtu kuzaliwa akiwa na asili ya dhambi, kila mtu anatenda dhambi pia. Hivyo watu wote pamoja, na wewe, wanazaliwa katika dhambi na pia wote wanatenda dhambi.

MHUBIRI 7:20:

“Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.”

ZABURI 53:3:

“Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja, hakuna atendaye mema, La! hata mmoja.”

ISAYA 53:6:

“Sisi sote kama kondoo tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe———”.

WARUMI 3:23:

“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”

WARUMI 5:12:

“Kwa hiyo kama kwa mtu mmoja (Adamu) dhambi iliingia ulimwenguni na kwa dhambi hiyo mauti na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”.

1 YOHANA 1:8, 10:

“Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.”

Unaona basi! Kila mtu anakuwa mwenye dhambi kutokana na uzao wa Adamu. Kila mtu anazaliwa akiwa ana asili ya dhambi. Kama Adamu alivyofanya dhambi, wote tunazaliwa na dhambi ya asili.

KANISA LA KILUTHERI MWANZA LATOA TAMKO JUU YA BOMU KANISANI KWAO


Kanisa la Kilutheri jijini Mwanza.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria (DMZV), limeitaka Serikali kuhakikisha inawatafuta watu waliohusika na tukio la bomu lililolipuka kanisani hapo juzi.Pia, limewataka Wakristo kuwa watulivu, wasiogope wala wasitishwe na mashambulizi hayo na kwamba wasilipize kisasi.

Akizungumza kwenye Kanisa la Imani Makongoro Misheni jana, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki Ziwa Victoria, Andrew Gulle alisema wanaamini shambulio hilo ni la kigaidi na kwamba, Serikali inapaswa kuchukua hatua ya kuwasaka wanaohusika “Kanisa tunaamini tukio hili linahusiana na ugaidi, umefika wakati Serikali ikachukua hatua za kuwasaka waliohusika ili sheria ifuate mkondo wake,” alisema Gulle.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya dini wanasema huenda tukio hilo linatokana na migogoro inayoendelea kanisani hapo kwa sababu tayari kuna baadhi ya waumini wamejitenga kwa kuanzisha kanisa lingine “Wasikwepe matatizo yao ya ndani, kuna askofu aliuawa kwa kupigwa tofali kutokana na migogoro, hivyo hata hili (tukio) litakuwa ni migogoro inayoendelea,” alisema mmoja wa waumini ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Askofu Gulle alikanusha kuwapo kwa migogoro kanisani hapo na kwamba, tukio hilo halihusiani na mgogoro wowote ndani ya Kanisa bali ni ugaidi.

Majeruhi aendelea vizuri

Hali ya majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea kanisani hapo, Benadeta Alfred, imeelezwa kuendelea vizuri katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikolazwa. “Hali ya mgonjwa ni nzuri ukilinganisha na tulivyompokea kwani hata kuongea alikuwa hawezi, lakini hivi sasa anaweza kuongea japo kwa shida,” alisema Lema.

Ijumaa, 2 Mei 2014

Je, Biblia Ina Habari Sahihi Kuhusu Maisha ya Yesu?


Jibu la Biblia
Mwandishi wa Biblia, Luka, alisema hivi kuhusu masimulizi aliyoandika kuhusu maisha ya Yesu: “nimefuata kwa uangalifu mambo yote tangu mwanzo kwa usahihi.”—Luka 1:3.

Watu fulani wanadai kwamba masimulizi ya maisha ya Yesu yaliyoandikwa katika Vitabu vya Injili, yaani, maandishi ya watu walioishi wakati wake kama vile Mathayo, Marko, Luka, na Yohana, yalibadilishwa wakati fulani katika karne ya nne.

Hata hivyo, sehemu fulani muhimu ya Injili ya Yohana ilipatikana nchini Misri mwanzoni mwa karne ya 20. Sehemu hiyo inajulikana kamaPapyrus Rylands 457 (P52) na imehifadhiwa katika Maktaba ya John Rylands Library, huko Manchester, Uingereza. Ina kitabu cha Yohana 18:31-33, 37, 38 katika Biblia za leo.

Hii ndiyo sehemu ya zamani zaidi ya hati za Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo. Wasomi wengi wanaamini kwamba sehemu hiyo iliandikwa karibu mwaka wa 125 W.K., miaka 25hivi baada ya maandishi ya awali kuandikwa. Maandishi ya sehemu hii yanalingana kabisa na maandishi ya hati za baadaye.

Kwa Nini Yesu Anaitwa Mwana wa Mungu?

Jibu la Biblia
Mungu hakuwa na mke halisi ambaye walipata naye watoto. Lakini ndiye Muumba wa vitu vyote. (Ufunuo 4:11) Kwa hiyo, Adamu, mwanadamu wa kwanza ambaye Mungu alimuumba, anaitwa “mwana wa Mungu.” (Luka 3:38) Vilevile, Biblia inafundisha kwamba Yesu aliumbwa na Mungu. Hivyo, Yesu pia anaitwa “Mwana wa Mungu.”—Yohana 1:49.

Mungu alimuumba Yesu kabla ya kumuumba Adamu. Kumhusu Yesu, Mtume Paulo aliandika: “Yeye ndiye mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.” (Wakolosai 1:15) Maisha ya Yesu yalianza miaka mingi kabla ya kuzaliwa katika zizi huko Bethlehemu. Hata Biblia inasema kwamba “asili yake ni kutoka nyakati za kale, kutoka siku za wakati usio na kipimo.” (Mika 5:2) Kabla ya kuzaliwa akiwa mwanadamu hapa duniani Yesu, Mwana mzaliwa wa kwanza wa Mungu, alikuwa kiumbe wa roho huko mbinguni. Yesu mwenyewe alisema hivi: “Nimeshuka kutoka mbinguni.”—Yohana 6:38

FIKRA NJE YA BOKSI: BADILI CHANZO CHA TAARIFA

chanzo gosipe Kitaa
Na Fredy Msungu

UTANGULIZI
Katika maisha ya kila siku, kila mmoja kwa upande wake kuna mambo ambayo anayatarajia sana kama matokeo halisi ya kitu fulani aliwahi kupanga au kuwaza katika maisha yake.Japo kua matarajio hayo hua ni siri ya mtu binafsi lakini nina uhakika kwa asilimia nyingi sana kwamba kila mmoja wetu anamatarajio mazuri katika maisha yake.Pamoja na kua kila mmoja wetu anategemea matokeo mazuri (chanya) lakini kuna kitu cha kwanza kufanya ambacho hicho ndio huleta matokeo unayoyahitaji,Inawezekana ukawa na matarajio mazuri sana lakini kua na matarajio (imani juu ya kitu fulani)na mambo makuu na mazuri hiyo haimaanishi tayari umepata uhakika au tiketi ya kuyafikia matarajio hayona kuyafanya kua kitu harusi.Wapo watu wengi waliokua na ndoto kubwa (matarajio)lakini hawakuweza kufikia, Na hii ni kwasababu tu!Hawakutengeza mwanzo wao kuakisi matokeo ya kesho yao.Kua na wazo au tarajio zuri peke yake si ufunguo wa mafanikio kuyafikia malengo, kuna mambo ambayo kupitia kwayo hayo ndio huzaa matokeo chanya moja kati ya jambo la msingi sana kati ya hayo ni CHANZO CHA TAARIFA:
TAARIFA NI NINI?Taarifa ni ujumbe wowote unaokujia kwa njia tofauti tofauti...inaweza kua kwa :-
• Kuambiwa /kusimuliwa
• Kusikiliza
• Kusoma
• Kuona

Viko vitu vingi ambavyo vinaweza kua ni sababu ya wewe kupata taarifa, lakini hizo ni njia au vyanzo vichache ambavyo mara nyingi vimetumika sana kutoa taarifa au elimu ya kitu fulani. Kitu cha muhimu Sana hapa kujua ni kwamba taarifa ni taarifa Haijalishi ni taarifa nzuri au mbaya!Ukishaipokea kwa kupitia moja kati ya hizo njia nilizoziorodhesha basi tayari hiyo ni taarifa.Na kwa namna moja au nyingine tegemea kuathiriwa na ile taarifa ulioipokea.

LENGO LA TAARIFA NI NINI?Lengo kuu la taarifa hua ni kujuza, kuaminisha, Kuonya, kuelimisha na wakati mwingine kupotosha .Hayo yote ni malengo ya taarifa ambayo mara nyingi yanatokea kutokana na mtoaji taarifa anamlengo gani au mpokeaji wa hiyo taarifa amechagua kusikia nini au kumsikiliza nani.
Kitaalamu, kiuumbaji (kisayansi) moja kati ya kazi kubwa ya ubongo ni kupokea taarifa mbali mbali (kufikiri) Na huwezi kufikiri bilakua na kitu cha kukifikiria, Sasa hicho kitu cha kufikiri ndio hiyo taarifa ambayo inatokana na vile vyanzo nilivyoviorodhesha awali.

MUHIMU: Ninachotaka kukujuza hapa ni kwamba uwe unapenda au haupendi swala la kupokea taarifa kwako si la hiyari kwako, Ni lazima kuna taarifa ubongo wako utapokea tu! na baada ya ubongo kupokea taarifa ni lazima ubongo ufanye kazi ya kufikiri, na fikra hutokea kutokana na aina ya taarifa uliyoisikia na matokeo yeyote unayoyaona yametokea nje chanzo chake hua ni taarifa.Swala kupokea taarifa si hiyari lakini ni aina ipi ya taarifa umechagua kupokea hilo ni uchaguzi wako.

Kwa maneno machace tu hapa naweza kukujuza kwamba ......CHANZO SAHIHI CHA TAARIFA HULETA FIKRA SAHIHI....NA FIKRA SAHIHI HULETA MATOKEO SAHIHI.vivyo hivyo CHANZO KIBOVU (POTOFU) CHA TAARIFA HULETA FIKRA MBOVU NA FIKRA MBOVU HULETA MATOKEO MABOVU

JINSI TAARIFA INAVYOATHIRI MAAMUZI YAKO
Maamuzi ni chanzo kikubwa cha matokeo, Hakuna jambo lolote lilitokea bila mtu kufanya maamuzi ya kuliweka jambo katika vitendo, Wazo pekee halitoshi kuleta matokeo yanayoonekana ...maamuzi ni hatua inayosababisha tendo na tendo huleta matokeo lakini haya maamuzi yanaathiriwa sana na chanzo cha taarifa. (Warumi 10:17 Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neon la kristo) Ukisoma Kwa umakini hapo utatambua kitu kikubwa sana. Ukifikia hatua ya kuamua kitu basi lazima kuna taarifa iliyokushawishi kukupelekea wewe kuamua.Imani ni matokeo tayari ambayo chanzo chake kimekuja kwa njia ya kusikia lakini chanzo cha taarifa hapa ni nini? Au kusikia kutoka kwenye chanzo gani cha taarifa? Hili ni swali kubwa ambalo unatakiwa kujiuliza.Kwa mujibu wa andiko hapo juu utaona kwamba kulisikia neno la kristo hicho ndo chanzo kikuu cha taaarifa.Sasa kama matokeo ya kuamini au imani hua ni kusikia jiadhari sana na nini unachagua kusikia kwani hicho ndicho huleta matokeo ya jambo.Unaweza ukawa unajiuliza sana kwanini mara nyingi katika safu hii nimetumia neno ‘UNACHAGUA KUSIKIA’?Kitu kikubwa ninaamini katika maisha hali yeyote ulionayo ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe,kama ni umasikini au utajiri,kufaulu au kufeli,kushinda ama kushindwa hivi vitu vyote ni uchaguzi wa mtu binafsi.Hii inaweza ikakupa shida kidogo lakini nitakueleza kwanini imani yangu inanituma hivyo.

FIKRA TATA: 1
• Hakuna mtu aliezaliwa na kitu/mali /mafanikio... Inaweza ikakupa shida kuamini kwasababu kila siku unaona kuna watu mashuhuri/matajiri na wana watoto, utaniambia Fred wale si watu waliozaliwa na kuyakuta mafanikio tayari? Ni sawa lakini hebu tulia kidogo na fikiri hivi yule mtu wa kwanza kabisa ambae ndio mwenye hayo mafanikio ...Je nayeye hizo mali/mafanikio alizitoa wapi? Jibu ni rahisi sana hapa kwamba wakati wote tulikua katika hali sawa uwezo sawa na mazingira sawa kuna mtu mmoja ambae yeye aliamua kufikiri zaidi ya mipaka ya kawaida (fikra nje ya boksi) Matokeo ya kufikiri nje ya mipaka ni kufanya vitu nje ya mipaka na kufanya vitu nje ya mipaka ni kupata matokeo makubwa nje ya mipaka.Baada ya hayo yote sasa utofauti ndio unaanza kuonekana kwasababu yeye aliamua kulipa gharama na kutenda nje ya mipaka ni lazima matokeo yamtoe nje ya mipaka pia na ndio maana watu wenye uwezu wa juu na wasio na uwezo hawakai sehemu moja..Unaweza ukalahumu saaana lakini mfumo ndo umeamua hivyo aliwaza nje ya mipaka ataishi nje ya mipaka pia, Lakini wote mwanzo wetu ulikua sawa.

AMKA MAISHA NI UCHAGUZI.
KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MALENGO/NDOTO NA TAARIFA?
Hili linaweza kua moja kati ya maswali ambayo umejiuliza sana toka ulipoanza kusoma safu hii, Kwamba mipango /ndoto ni yako wewe binafsi sasa taarifa inaingiaje hapa ama kuna uhusiano gani baina ya vitu hivi viwili?

Jibu: Ni kweli kwamba maisha ni yako wewe ndoto/mipango na maono uliyonayo ni vyako.Lakini kumbuka mpaka vitu hivyo vikatokee kuna mchakato fulani ambao ni lazima uupitie kama njia ya kuielekea hatma yako au kilele cha mafanikio yako.
Njia hizo ni:-
• Kujifunza/kupata uzoefu: Sehemu yeyote duniani kwenye sekta yeyote hakuna mtu ambaye amefanikiwa na akasema kwamba hakuna mtu yeyote mwenye mchango katika mafanikio yake, abadani si kweli.... mara zote hua kuna watu waliotutangulia (wenye uzoefu)ambao wamefanya vitu sawa na tunavyoviwaza wakafanikawa, watu hao husimama kama mifano/ushuhuda kwa vizazi vingine vijavyo ili kuyafikia malengo.Kama kumbu kumbu yako nzuri utakumbuka mwanzoni kabisa nilikuambia kwamba jitambue wewe ni nani na unataka nini ili uchague watu unaodhani wanafanana na wewe ili upate uzoefu(kujifunza toka kwao)Ili kuyafikia matokeo unayoyatarajia.Na uzoefu huo utaupata kwa njia ya kujifunza.

Kuna njia nyinginezo nyingi ambazo ni vyanzo vya taarifa, Na huu ndio uhusiano sasa kati ya ndoto yako/malengo/mipango na taarifa. Taarifa inaathiri Sana matokeo ya malengo yako kwasababu wakati wa kutendea kazi mawazo unazungukwa ka watu mbali mbali na pengine ili kufikia malengo itakuhitaji pia kuwatumia baadhi ya watu ili kutoboza upande wa pili na hii ndio sababu unatakiwa kua na chanzo sahihi cha taarifa ili usikie vitu sahihi.

UMECHAGUA FUNGU GANI LA TAARIFA?
Kama swala la kusikia! Watu wengi wanasikia.....Ila unasikia nini? Kutoka Kwa nani? Hapa ndio nataka kujenga hoja yangu Kwa upana kwasababu chochote ulichoamini mwanzo wake ulikua ni kusikia. Baada ya kusikia na kuamini maamuzi ya vitendo hufuata.Na hapa ndipo safari ya mafanikio au ya kufeli (kutofanikiwa)inaanza.Na hii inatokana umesikia taarifa gani kutoka kwenye chanzo gani uliochagua kuisikiliza na kuiamini.Ukisikia taarifa sahihi utaamua kwa jinnsi ilivyo sahihi ,Pia ukisikia kwa taarifa isiyo sahihi kutoka kwenye chanzo kisicho sahihi basi fikra na maamuzi yako pia hayatakua sahihi.Inawezekana kabisa ukaona ukuu ndani yako ukawa na mipango mikubwa tu , lakini kama utaruhusu masikio na fikra yako kupokea taarifa za kushindwa mara kwa mara, haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani ukiruhusu taarifa za kushindwa tegemea kushindwa pia.

Kabla sijatoa mfano huu nikuweke sawa kwanza katika hili...Kwagu mimi kiwango cha utajiri wa mtu au mafanikio makubwa ya aina yeyote si kigezo kwamba Mungu ndio anatenda kazi au niamini Mungu kwasababu amefany litu fulani,Nimefika mahali pa kuelewa kua Mungu hua anabaki kua Mungu tu iwe ametenda unachotaka au hajatenda..(Mungu hapimwi kwa alichofanya anabaki kua Mungu kwasababu ndivyo alivyo) huo ni mtazamo wangu, Japo kua mimi siamini katika umasikini
Sasa mfano wangu ni huu..!Ukifanya tathinimi ya wale wachungaji ambao wao wanahubiri sana injili za aina moja unyonge (uhitaji) hebu jaribu kuangalia maisha yao na ya watu wanaowaongoza...hali zao kiuchumi (kimaisha)hua ni mbaya sana na wao hua wameridhika kabisa, Lakini si kwamba Mungu hawezi kufanya kitu au hawana Mungu hapana! Ila kwasababu ni kitu ambacho wanakisikia kwa sana,Hivyo inawajengea imani na imani inaleta matokeo ya walichokisia.Kwahiyo hili si swala la kumlaumu mtu ni swala la ufahamu tu...Baba wa upentecoste Nigeria Askofu mkuu Benson Idahosa enzi za uhai wake aliwahi kusema hivi ‘Ukihubiri sana juu ya habari ya kuzimu(moto) kuna hatari kubwa washirika wako wakaishia huko,Lakini ukihubiri sana juu ya habari za mbinguni kuna asilimia kubwa ya watu unaowaongoza kuiona mbingu(peponi)’.Kauli hii ilinigusa sana na imeakisi sana ujumbe wangu kwamba chanzo cha taarifa kikiwa kibaya mara kwa mara tegemea matokeo mabaya na pia ukijizoesha kusikiliza taarifa za ushindi tegemea ushindi pia.

Hata katika maisha yetu ya kawaida kabisa kuna watu wengi waliamua kufanya vitu kutokana na taarifa fulani waliosikia kwa wengine. Aina hii ya taarifa tunaweza kuiita ni ushuhuda. Mfano: Watu wengi katika biashara ya simu mara nyingi wanahama katika mitando yao kwenda mitandao mingine kwasababu ya kusikia taarifa(ushuhuda)toka kwa mwingine kwamba huku kuna nafuu kuliko sehemu nyingine.Kinachomfanya huyu mtu kufanya maamuzi ya kuhama ni ile taarifa (ushuhuda)aliyoipata kutoka kwa mwingine,Hivyo maamuzi yake yameathiriwa na taarifa aliyoisikia.

Mfano: 2 Watu wengi sasa wanaamua kuondoka vijijini kukimbilia mjini kutokana na taarifa wanazozipata kwamba mjini kuna maisha mazuri kuliko kijijni.Inawezekana ikawa si taarifa sahihi lakini tayari mtu kashafanya maamuzi kutokana na aina ya taarifa aliyoipata.Hata makanisani watu wanahama kutokana na taarifa wanazozipata zinazowapelekea wao kuamini kwamba kuna matokeo tofauti atakayoyapata, Haijalishi kama lengo hua linatimia au halitimii....kikubwa hapa ni kwamba kitu kilichomsababisha mtu kufanya maamuzi aliyofanya ni ile taarifa aliyoipata.


Tuendelee wiki ijayo...
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0653-318117, ama kwa barua pepe fredymsungu@gmail.com

Alhamisi, 1 Mei 2014

TAFSIRI YA NAMBA 5 KATIKA MAANDIKO


Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa The Voice of Hope Ministries (VHM).

Namba TANO ni namba ya neema ya maajabu ya Mungu.
Nakutakia Neema na Maajabu ya Mungu katika MWezi huu wa 5

1. Mwanzo 1:20, 21 tunasoma udhihirisho wa neema ya Mungu katika kuumba. Aliumba viumbe hai katika siku ya TANO.
2. Katika Mwanzo 15:9, Mungu aliagiza wanyama WATANO wachinjwe.
3. Isaya 9:6 inamtaja Yesu katika nafsi TANO, (Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani).
4. Yesu aliwalisha watu zaidi ya elfu TANO na mikateilikuwa MITANO.
(Mt 15:13
5. Waefeso 4:11, Kristo alitoa huduma TANO kwa Kanisa. (Mitume, Manabii, Wachungaji, Wainjilisti na Waalimu.
6. Katika Mambo ya Walawi waliamriwa kutoa sadaka za aina TANO. (Sadaka ya Ondoleo la Dhambi, Sadaka ya Asili, Sadaka ya Matendo ya Dhambi, Sadaka ya Amani).
7. Kulikuwa na wanawali wa TANO wenye busara na WATANO wapumbavu
8. (Mt 25:34)
9. Namba TANO imetajwa mara 318 katika maandiko.
10. Amri 10 zimegawanyika katika mafungu mawili, amri TANO za kwanza zinazungumzia juu ya uhusiano wetu na Mungu, na amri TANO zingine zinazungumzia juu ya uhusiano wetu sisi kwa sisi.
11. Katika agano la kale mwizi lazima alipe mara TANO ya thamani ya mifugo aliyoiba.(Kutoka 22:1)
1 “Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja”
Nawewe kila ambacho shetani ameiba mwezi huu lazima arudishe mara tano ya thamani yake sema amen.

13. Benjamin aliheshimiwa na Yusufu kwa kupewa nafaka mara TANO zaidi ya kaka zake. (Mwanzo 43:34)
“34 Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara TANO kuliko zao. Wakanywa, wakafanya furaha pamoja naye.”

14. Namba Tano inawakirisha Neema ya Mungu na hii inaonekana katika muundo wa hema ya kukutania kule jangwani. (Kutoka Sura ya 26)
• Nguzo zilikuwa dhiraa TANO mbali na mikono mitano ya juu.

• Madhabahu ya shaba ilikuwa mikono MITANO kwa mikono mitano.

• Kulikuwa na nguzo TANO mwishoni mwa Patakatifu.

• Pande za maskani zilikuwa kushinikizwa na baa TANO kila upande (Kutoka 26:26-27)
Nawe fanya mataruma ya mti wa mshita; mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani, 27 na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi.

• Mfuniko wa ndani mwa hema ulikuwa na mapazia matano ambayo yaliambatanishwa na mapazia MATANO mengine na kufanya jumla ya mapazia 10. (Kutoka 26:3)
3 Mapazia matano yataungwa pamoja, hili na hili; na mapazia MATANO mengine yataungwa pamoja, hili na hili.”

• Kulikuwa na makuhani halisi watano Haruni na watoto wake wanne (Kutoka 28:1)
“Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni.”

15. Kulikuwa na Matao TANO katika lile birika la Bethaida. (Yohana 5:2)
2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano

16. Kitabu cha Zaburi kimegawanyika katika sehemu huu TANO
• Zaburi 1- 41
Inahusu sikukuu ya Pasaka, mwanzo wa Israeli, na mwanzo wa mpango wa Mungu wa wokovu kuelekea Kristo.

• Zaburi 42 – 72
Inahusu juu ya ishara ya umoja wa Israel katika ardhi na inatoa picha ya uumbaji wa kanisa la Agano jipya.
• Zaburi 73 – 89
Laana juu ya uharibifu wa hekalu la Mungu na mji wa Yerusalem. Sehemu hii pia inazungumzia juu ya siku za mwisho na dhiki kuu.

• Zaburi 90 – 106
Kufurahia zaidi ya 1,000 ya utawala wa Yesu na inaonyesha Israeli walikutana tena

• Zaburi 107 – 150
Inatoa picha ya wakati ambapo Yuda (mwakilishi wa Israel) atakapokombolewa tena.

KAMA UMEBARIKIWA SEMA AMEN!