chanzo gosipe Kitaa
Na Fredy Msungu
UTANGULIZI
Katika maisha ya kila siku, kila mmoja kwa upande wake kuna mambo ambayo anayatarajia sana kama matokeo halisi ya kitu fulani aliwahi kupanga au kuwaza katika maisha yake.Japo kua matarajio hayo hua ni siri ya mtu binafsi lakini nina uhakika kwa asilimia nyingi sana kwamba kila mmoja wetu anamatarajio mazuri katika maisha yake.Pamoja na kua kila mmoja wetu anategemea matokeo mazuri (chanya) lakini kuna kitu cha kwanza kufanya ambacho hicho ndio huleta matokeo unayoyahitaji,Inawezekana ukawa na matarajio mazuri sana lakini kua na matarajio (imani juu ya kitu fulani)na mambo makuu na mazuri hiyo haimaanishi tayari umepata uhakika au tiketi ya kuyafikia matarajio hayona kuyafanya kua kitu harusi.Wapo watu wengi waliokua na ndoto kubwa (matarajio)lakini hawakuweza kufikia, Na hii ni kwasababu tu!Hawakutengeza mwanzo wao kuakisi matokeo ya kesho yao.Kua na wazo au tarajio zuri peke yake si ufunguo wa mafanikio kuyafikia malengo, kuna mambo ambayo kupitia kwayo hayo ndio huzaa matokeo chanya moja kati ya jambo la msingi sana kati ya hayo ni CHANZO CHA TAARIFA:
TAARIFA NI NINI?Taarifa ni ujumbe wowote unaokujia kwa njia tofauti tofauti...inaweza kua kwa :-
• Kuambiwa /kusimuliwa
• Kusikiliza
• Kusoma
• Kuona
Viko vitu vingi ambavyo vinaweza kua ni sababu ya wewe kupata taarifa, lakini hizo ni njia au vyanzo vichache ambavyo mara nyingi vimetumika sana kutoa taarifa au elimu ya kitu fulani. Kitu cha muhimu Sana hapa kujua ni kwamba taarifa ni taarifa Haijalishi ni taarifa nzuri au mbaya!Ukishaipokea kwa kupitia moja kati ya hizo njia nilizoziorodhesha basi tayari hiyo ni taarifa.Na kwa namna moja au nyingine tegemea kuathiriwa na ile taarifa ulioipokea.
LENGO LA TAARIFA NI NINI?Lengo kuu la taarifa hua ni kujuza, kuaminisha, Kuonya, kuelimisha na wakati mwingine kupotosha .Hayo yote ni malengo ya taarifa ambayo mara nyingi yanatokea kutokana na mtoaji taarifa anamlengo gani au mpokeaji wa hiyo taarifa amechagua kusikia nini au kumsikiliza nani.
Kitaalamu, kiuumbaji (kisayansi) moja kati ya kazi kubwa ya ubongo ni kupokea taarifa mbali mbali (kufikiri) Na huwezi kufikiri bilakua na kitu cha kukifikiria, Sasa hicho kitu cha kufikiri ndio hiyo taarifa ambayo inatokana na vile vyanzo nilivyoviorodhesha awali.
MUHIMU: Ninachotaka kukujuza hapa ni kwamba uwe unapenda au haupendi swala la kupokea taarifa kwako si la hiyari kwako, Ni lazima kuna taarifa ubongo wako utapokea tu! na baada ya ubongo kupokea taarifa ni lazima ubongo ufanye kazi ya kufikiri, na fikra hutokea kutokana na aina ya taarifa uliyoisikia na matokeo yeyote unayoyaona yametokea nje chanzo chake hua ni taarifa.Swala kupokea taarifa si hiyari lakini ni aina ipi ya taarifa umechagua kupokea hilo ni uchaguzi wako.
Kwa maneno machace tu hapa naweza kukujuza kwamba ......CHANZO SAHIHI CHA TAARIFA HULETA FIKRA SAHIHI....NA FIKRA SAHIHI HULETA MATOKEO SAHIHI.vivyo hivyo CHANZO KIBOVU (POTOFU) CHA TAARIFA HULETA FIKRA MBOVU NA FIKRA MBOVU HULETA MATOKEO MABOVU
JINSI TAARIFA INAVYOATHIRI MAAMUZI YAKO
Maamuzi ni chanzo kikubwa cha matokeo, Hakuna jambo lolote lilitokea bila mtu kufanya maamuzi ya kuliweka jambo katika vitendo, Wazo pekee halitoshi kuleta matokeo yanayoonekana ...maamuzi ni hatua inayosababisha tendo na tendo huleta matokeo lakini haya maamuzi yanaathiriwa sana na chanzo cha taarifa. (Warumi 10:17 Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neon la kristo) Ukisoma Kwa umakini hapo utatambua kitu kikubwa sana. Ukifikia hatua ya kuamua kitu basi lazima kuna taarifa iliyokushawishi kukupelekea wewe kuamua.Imani ni matokeo tayari ambayo chanzo chake kimekuja kwa njia ya kusikia lakini chanzo cha taarifa hapa ni nini? Au kusikia kutoka kwenye chanzo gani cha taarifa? Hili ni swali kubwa ambalo unatakiwa kujiuliza.Kwa mujibu wa andiko hapo juu utaona kwamba kulisikia neno la kristo hicho ndo chanzo kikuu cha taaarifa.Sasa kama matokeo ya kuamini au imani hua ni kusikia jiadhari sana na nini unachagua kusikia kwani hicho ndicho huleta matokeo ya jambo.Unaweza ukawa unajiuliza sana kwanini mara nyingi katika safu hii nimetumia neno ‘UNACHAGUA KUSIKIA’?Kitu kikubwa ninaamini katika maisha hali yeyote ulionayo ni matokeo ya uchaguzi wako mwenyewe,kama ni umasikini au utajiri,kufaulu au kufeli,kushinda ama kushindwa hivi vitu vyote ni uchaguzi wa mtu binafsi.Hii inaweza ikakupa shida kidogo lakini nitakueleza kwanini imani yangu inanituma hivyo.
FIKRA TATA: 1
• Hakuna mtu aliezaliwa na kitu/mali /mafanikio... Inaweza ikakupa shida kuamini kwasababu kila siku unaona kuna watu mashuhuri/matajiri na wana watoto, utaniambia Fred wale si watu waliozaliwa na kuyakuta mafanikio tayari? Ni sawa lakini hebu tulia kidogo na fikiri hivi yule mtu wa kwanza kabisa ambae ndio mwenye hayo mafanikio ...Je nayeye hizo mali/mafanikio alizitoa wapi? Jibu ni rahisi sana hapa kwamba wakati wote tulikua katika hali sawa uwezo sawa na mazingira sawa kuna mtu mmoja ambae yeye aliamua kufikiri zaidi ya mipaka ya kawaida (fikra nje ya boksi) Matokeo ya kufikiri nje ya mipaka ni kufanya vitu nje ya mipaka na kufanya vitu nje ya mipaka ni kupata matokeo makubwa nje ya mipaka.Baada ya hayo yote sasa utofauti ndio unaanza kuonekana kwasababu yeye aliamua kulipa gharama na kutenda nje ya mipaka ni lazima matokeo yamtoe nje ya mipaka pia na ndio maana watu wenye uwezu wa juu na wasio na uwezo hawakai sehemu moja..Unaweza ukalahumu saaana lakini mfumo ndo umeamua hivyo aliwaza nje ya mipaka ataishi nje ya mipaka pia, Lakini wote mwanzo wetu ulikua sawa.
AMKA MAISHA NI UCHAGUZI.
KUNA UHUSIANO GANI KATI YA MALENGO/NDOTO NA TAARIFA?
Hili linaweza kua moja kati ya maswali ambayo umejiuliza sana toka ulipoanza kusoma safu hii, Kwamba mipango /ndoto ni yako wewe binafsi sasa taarifa inaingiaje hapa ama kuna uhusiano gani baina ya vitu hivi viwili?
Jibu: Ni kweli kwamba maisha ni yako wewe ndoto/mipango na maono uliyonayo ni vyako.Lakini kumbuka mpaka vitu hivyo vikatokee kuna mchakato fulani ambao ni lazima uupitie kama njia ya kuielekea hatma yako au kilele cha mafanikio yako.
Njia hizo ni:-
• Kujifunza/kupata uzoefu: Sehemu yeyote duniani kwenye sekta yeyote hakuna mtu ambaye amefanikiwa na akasema kwamba hakuna mtu yeyote mwenye mchango katika mafanikio yake, abadani si kweli.... mara zote hua kuna watu waliotutangulia (wenye uzoefu)ambao wamefanya vitu sawa na tunavyoviwaza wakafanikawa, watu hao husimama kama mifano/ushuhuda kwa vizazi vingine vijavyo ili kuyafikia malengo.Kama kumbu kumbu yako nzuri utakumbuka mwanzoni kabisa nilikuambia kwamba jitambue wewe ni nani na unataka nini ili uchague watu unaodhani wanafanana na wewe ili upate uzoefu(kujifunza toka kwao)Ili kuyafikia matokeo unayoyatarajia.Na uzoefu huo utaupata kwa njia ya kujifunza.
Kuna njia nyinginezo nyingi ambazo ni vyanzo vya taarifa, Na huu ndio uhusiano sasa kati ya ndoto yako/malengo/mipango na taarifa. Taarifa inaathiri Sana matokeo ya malengo yako kwasababu wakati wa kutendea kazi mawazo unazungukwa ka watu mbali mbali na pengine ili kufikia malengo itakuhitaji pia kuwatumia baadhi ya watu ili kutoboza upande wa pili na hii ndio sababu unatakiwa kua na chanzo sahihi cha taarifa ili usikie vitu sahihi.
UMECHAGUA FUNGU GANI LA TAARIFA?
Kama swala la kusikia! Watu wengi wanasikia.....Ila unasikia nini? Kutoka Kwa nani? Hapa ndio nataka kujenga hoja yangu Kwa upana kwasababu chochote ulichoamini mwanzo wake ulikua ni kusikia. Baada ya kusikia na kuamini maamuzi ya vitendo hufuata.Na hapa ndipo safari ya mafanikio au ya kufeli (kutofanikiwa)inaanza.Na hii inatokana umesikia taarifa gani kutoka kwenye chanzo gani uliochagua kuisikiliza na kuiamini.Ukisikia taarifa sahihi utaamua kwa jinnsi ilivyo sahihi ,Pia ukisikia kwa taarifa isiyo sahihi kutoka kwenye chanzo kisicho sahihi basi fikra na maamuzi yako pia hayatakua sahihi.Inawezekana kabisa ukaona ukuu ndani yako ukawa na mipango mikubwa tu , lakini kama utaruhusu masikio na fikra yako kupokea taarifa za kushindwa mara kwa mara, haijalishi una ndoto kubwa kiasi gani ukiruhusu taarifa za kushindwa tegemea kushindwa pia.
Kabla sijatoa mfano huu nikuweke sawa kwanza katika hili...Kwagu mimi kiwango cha utajiri wa mtu au mafanikio makubwa ya aina yeyote si kigezo kwamba Mungu ndio anatenda kazi au niamini Mungu kwasababu amefany litu fulani,Nimefika mahali pa kuelewa kua Mungu hua anabaki kua Mungu tu iwe ametenda unachotaka au hajatenda..(Mungu hapimwi kwa alichofanya anabaki kua Mungu kwasababu ndivyo alivyo) huo ni mtazamo wangu, Japo kua mimi siamini katika umasikini
Sasa mfano wangu ni huu..!Ukifanya tathinimi ya wale wachungaji ambao wao wanahubiri sana injili za aina moja unyonge (uhitaji) hebu jaribu kuangalia maisha yao na ya watu wanaowaongoza...hali zao kiuchumi (kimaisha)hua ni mbaya sana na wao hua wameridhika kabisa, Lakini si kwamba Mungu hawezi kufanya kitu au hawana Mungu hapana! Ila kwasababu ni kitu ambacho wanakisikia kwa sana,Hivyo inawajengea imani na imani inaleta matokeo ya walichokisia.Kwahiyo hili si swala la kumlaumu mtu ni swala la ufahamu tu...Baba wa upentecoste Nigeria Askofu mkuu Benson Idahosa enzi za uhai wake aliwahi kusema hivi ‘Ukihubiri sana juu ya habari ya kuzimu(moto) kuna hatari kubwa washirika wako wakaishia huko,Lakini ukihubiri sana juu ya habari za mbinguni kuna asilimia kubwa ya watu unaowaongoza kuiona mbingu(peponi)’.Kauli hii ilinigusa sana na imeakisi sana ujumbe wangu kwamba chanzo cha taarifa kikiwa kibaya mara kwa mara tegemea matokeo mabaya na pia ukijizoesha kusikiliza taarifa za ushindi tegemea ushindi pia.
Hata katika maisha yetu ya kawaida kabisa kuna watu wengi waliamua kufanya vitu kutokana na taarifa fulani waliosikia kwa wengine. Aina hii ya taarifa tunaweza kuiita ni ushuhuda. Mfano: Watu wengi katika biashara ya simu mara nyingi wanahama katika mitando yao kwenda mitandao mingine kwasababu ya kusikia taarifa(ushuhuda)toka kwa mwingine kwamba huku kuna nafuu kuliko sehemu nyingine.Kinachomfanya huyu mtu kufanya maamuzi ya kuhama ni ile taarifa (ushuhuda)aliyoipata kutoka kwa mwingine,Hivyo maamuzi yake yameathiriwa na taarifa aliyoisikia.
Mfano: 2 Watu wengi sasa wanaamua kuondoka vijijini kukimbilia mjini kutokana na taarifa wanazozipata kwamba mjini kuna maisha mazuri kuliko kijijni.Inawezekana ikawa si taarifa sahihi lakini tayari mtu kashafanya maamuzi kutokana na aina ya taarifa aliyoipata.Hata makanisani watu wanahama kutokana na taarifa wanazozipata zinazowapelekea wao kuamini kwamba kuna matokeo tofauti atakayoyapata, Haijalishi kama lengo hua linatimia au halitimii....kikubwa hapa ni kwamba kitu kilichomsababisha mtu kufanya maamuzi aliyofanya ni ile taarifa aliyoipata.
Tuendelee wiki ijayo...
Unaweza kuwasiliana na mwandishi kupitia namba 0653-318117, ama kwa barua pepe fredymsungu@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni